1.Igor Akinfeev. Baada ya kuruhusu mabao katika michezo 43 iliyopita, mchezo wake wa jana ulikuwa mchezo wake wa kwanza kucheza bila kufungwa, lakini alionesha kiwango kikubwa sana na kuisaidia CSKA Moscow kushinda bao 2 kwa nunge.
2.Michael Lang. Aliwachefua kabisa Manchester United katika upande wa kulia, uwezo wa mlinzi huyu ulikuwa kikwazo kwa United. Alikuwa na uwezo mkubwa kupandisha mashambulizi na mara nyingi alionekana kumzidi maarifa Daley Blind.
3.Filipe Luiz. As Roma wako vizuri sana msimu huu lakini hana Atletico Madrid walionekama kuwazima kabisa, huku upande wa kushoto wa Atletico ukiwa imara zaidi kutoka na uwepo wa Fellipe Luiz.
4.Samuel Umtiti. Mlinzi wa kati wa klabu ya Barcelona alikuwa katika kiwango kikubwa na kufanikiwa kuwazuia washambuliaji wa Juventus kuwadhuru, kiwango cha Umtiti cha jana kimedhihirisha alistahili kuwa Barcelona.
5.Eric Dier. Maurcio Pochettino anaonekana anawajua haswa wachezaji wake na kwa mara nyingine anamshusha Dier katika nafasi ya mlinzi wa kati, na Dier ameonesha uwezo uliowafanya watu wengi kuamini kwamba ni kiraka haswa.
6.Ever Benega. Wengi wanajadili suluhu ya bao 3 kwa 3 kati ya Liverpool na Sevilla huku kila mmoja akitoa sababu, lakini Benega alikuwa kirusi kikubwa kwa Liverpool na kipindi cha pili aliwafanya Liverpool waonekane hawajui wanachofanya katika eneo la la kiungo.
7.Naby Keita. Uwezo wa kiungo huyu katika siku za hivi karibuni umekuwa gumzl dunia nzima, kwa mara nyingine Keita anaionesha dunia kwamba yeye ni kiungo wa kiwango cha dunia, aliwazima kabisa FC Monaco katika mchezo wao na RB Leizpg wakashinda bao 4 kwa moja.
8.Cesc Fabregas. Huyu ndiye “pass master” ana uwezo mkubwa mnoo na mchezo zidi ya Quarabag jicho lake na uwezo wa miguu yake vilitosha kwa UEFA kumuweka katika kikosi bora cha Champions League wiki hii.
9.Lorenzo Isingne. Uwezo mkubwa sana alioonesha zidi ya Shaktar Donetski umewafanya Waitaliano kuhoji sababu ya Gian Piero Ventura kumuweka nje katika mechi ambayo Italia walikatishwa ndoto zao za kwenda kombe la dunia.
10.Bas Dost. Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uholanzi alikuwa katika kiwango kikubwa sana wakati Sporting Lisbon wakiichapa Olympiakos kwa mabao 3 kwa 1 huku Bas Dost akifunga mabao mawili kwa kila kipindi.
11.Neymar. Achana na Edison Cavanni lakini mshambuliaji wa Kibrazil Neymar amezidi kuionesha dunia kwamba yeye anastahili kuwa mchezaji ghali duniani, alifunga mabao 2 wakati PSG wakishinda mabao 7 lakini alikuwa nyota katika mchezo huo.