Mkurugenzi Mkuu wa Acacia nchini Tanzania Brad Gordon na Mkurugenzi Mkuu wa fedha Andrew Wray, wamejiuzulu nyadhifa zao ingawa bado watakuwa chini ya kampuni mpaka mwisho wa mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa leo na kampuni hiyo na kusema kwamba Mkurugenzi Mkuu Brad Gordon anarejea nyumbani kwake Australia na Andrew Wray anatafuta fursa mahali kwengine.
Tayari Bodi ya Acacia imewataja watu ambao watachukua nyadhifa za wawili hao, ambao ni Peter Geleta ambaye atakuwa Mkurugenzi Mkuu na Jaco Maritz atakachukua nafasi ya Andrew Wray aliyekuwa Mkurugenzi wa fedha.
Peter ambaye ametajwa kuwa na uzoefu kwenye uchimbaji madini kwa muda wa miaka 35 ameshawahi kufanya kazi na mgodi wa Anglo Gold Ashanti kwa miaka 25 na kampuni ya Barrick, na alijiunga na Acacia mwaka 2012 na alishawahi kuwa Meneja Mkuu kwenye mgodi wa Bulyanhulu.
Acacia imewashukuru viongozi waliojiuzulu Brad Gordon na Andrew Wray kwa muda wao wote waliokuwa hapo huku wakisema walifanya nao kazi vizuri, na kuwatakia heri huko waendako, huku wakiamini waliochukua nafasi yao watafanya kazi kama ambavyo inastahili.
Ni lazima hawa tueazuie Na watusaudie ktk upelelezi WA kulitua yaifa hasara Na kuwanunua wana sasa kuwatetea Na kulihararisha taiga Na usalama wake.
ReplyDeleteAcacia kwa Tanzania iwe ni Historia.
ReplyDeleteBango hili linashushwa na mkataba utatiwa na Baliki au Jina pendekezi watakalo litoa.
Lakini kabla ya kufikia hatua hiyo.
ni lazima iwe regulated process overall.
Na hawa magumashi wasiruhusiwe kuondoka.mpaka tupate usaidizi katika mlolongo na mbinu walizo tumia na wamemlisha nani mpaka kutaka kuliingiza Taifa katika machafuko ya kikamii na kusababisha Hasara kubwa ambayo imeweza kunyamaziwa na vyomno husika ikiwemo TMAA / TRA / TPA / TCAA na mlolongo mzima wa Watanzania wakiwemo Makada wa uongozi kufumbia Macho. na wanasheria .
isingekuwa Magu nchii ingeendelea kupigwa na wanasiasa wa kuwasaidia Mabepari wangeendelea na kelele zao kama alivyosema MAREHEMU BABA WA TAIFA
HUYO HUYO HUYO HUYO.
Tusiwaachie waondoke mpaka tumeridhika na tumeupata mchongo wote na TAKUKURU IINGIE KAZI NA UHAMIAJI PIA.
MUngu mbariki JPJM na mungu ibariki Tanzania na Barrick Gold na wazalendo wetu kina PROF .KABUDI ( Mzelelo wa kukaya)
Prof Osoro Nehemia na Prof Abdulkadir Mruma na washiriki wa team zao including Prof John Thornton.
PCCB FANYENI KAZI TULIYO WAPA.
TANZANIA NI SALAMA NA IKO IMARA.
RASILI MALI NI LAZIMA ZINUFAISHE TAIFA