Klabu ya Simba Imewatunuku Wachezaji Wake Mapumziko Mafupi

Klabu ya Simba Imewatunuku Wachezaji Wake Mapumziko Mafupi
Baada ya kuchomoza na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na kurejea Dar es Salaam klabu ya soka ya Simba imetoa mapumziko mafupi kwa kikosi chake kabla ya kurudi tena katika majukumu yake hapo kesho.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram klabu ya Simba imesema mapumziko hayo mafupi ni ya siku moja pekee.

“Mapumziko: Kikosi cha Simba kiko katika mapumziko mafupi hii leo ambayo yatafuatiwa na muendelezo wa mazoezi kesho tarehe 21 Novemba 2017.” Imesema klabu ya Simba

Simba SC mpaka sasa inaongoza ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuwa na jumla ya pointi 22 wakati  Azam FC ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na alama 22 huku Yanga SC ikiwa ya tatu katika msimamo ikiwa na pointi 20.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad