Kubenea Awachoma Mafisadi

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage amesema wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki waliobinafsisha kiwanda hicho na kuiingizia hasara serikali watashughulikiwa ipasavyo.

Mwijage ameyasema hayo bungeni leo wakati akijibu maswali mawili ya nyongeza yaliyoulizwa na mbunge wa Ubungo Mh. Said Kubenea aliyetaka kujua hatua watakazo chukuliwa wafanyakazi walioshiriki kubinafsisha kiwanda cha urafiki kwa mwekezi kutoka China ambaye ameshindwa kuleta faida.
“Ukiiona ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG utalia Kubenea, kwahiyo kila mtu aliyehusika kutuingiza kwenye dhahama hii rungu litamshukia kama Mwewe”, amesema Waziri Mwijage
.
Aidha Waziri amesema kuwa tayari serikali ipo mbioni kumaliza makubaliano na mwekezaji mpya kutoka China ambapo kiwanda hicho kitajengwa upya vizuri na serikali itanufaika kwa takribani asilimia 75.
Waziri Mwijage ameongeza kuwa kiwanda cha Urefiki ni cha kihistoria hivyo watakijenga upya na kitakuwa na wafanyakazi zaidi ya elfu nane.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Muanze na Mkapa Kwanza. Ni CCM, mnawafanya Wachina marafiki. Wengi wachina hawana hata kisomo, hawana pesa, hawana uzalendo. Wanarangi nyekundu. maraisi waliowaingiza wachina kama wajomba zao. Na bado mnapokea misaada mingi toka Ucgina. Hizi ni hongo pia za kufunga midomo ya Watanzania. Hizi pikpiki makopo, wengine wanajengewa viwana na majumba, zote hizi ni hongo ndani ya serikali. Wanavyohamisha Wachina kutoka Tanzania bure huko vijijini, msingepokea visenti. Sheria mbovu ndizo zinaangamiza Taifa. Tunahitaji maarifa si vitu vya bure, hakuna cha bure. Mtegemea cha nduguye hufa hali maskini. upate elimu ujitegemee na uwe na heshima ndani ya nchi yako. mpokea misaada kila kitu unakuwa less of human being kuliko na mtoaji. Ndo unakosa sauti ndani ya nchi yako.
    Kuna dada toka Zambia, Dambisa Moyo aliandika kitabu kuhusu tegemezi la Africa kupata misaada toka nje zinaua maendeleo ya nchi. Alikuwa tayari kutoa free copies kwa maraisi wa africa na kueneza mashuleni, Maraisi wengi wa Africa walikataa. Akili ni mali.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad