"Kuichagua CCM ni Kufurahia Mateso" - Tundu Lissu

Mbunge Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu ametuma ujumbe kwa wapiga kura kwenye kata zenye uchaguzi ya kwamba kuwapatia kura za ushindi Chama Cha Mapinduzi ni kufurahia na kuruhusu mateso.

Ujumbe huo kutoka kwa Lissu kwenda kwa wapiga kura umefikishwa na Diwani wa Sombetini  Arusha, Ally Bananga ambaye amefika hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu mbunge huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bananga ameandika, "Nendeni mkawaambie watu kwenye kata zenye uchaguzi kuipa kura ccm ni kufurahia na kuruhusu mateso yetu yaendelee!!...."  Ujumbe alioutoa Lissu kupitia diwani Bananga

Ameongeza kwamba 'Hawa watesi wetu wako katika hatua za mwisho, kama wanajiamini kwa nn wanawawekea mizengwe wagombea wetu ili wao wapite bila kupingwa"

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad