Lazima Kuvuna Poindi Tatu kwa Mbeya City Bila Tshishimbi - Lwandamina

Lazima Kuvuna Poindi Tatu kwa Mbeya City Bila Tshishimbi - Lwandamina
LICHA ya kukosekana kwa kiungo wake nyota Papy Tshishimbi kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City, Kocha wa Yanga George Lwandamina amesisitiza kikosi chake kitaibuka na ushindi.

Akizungumza na Nipashe, Lwandamina, alisema kuwa mchezo wa kesho ni muhimu kwao kushinda hivyo hata asipokuwepo nyota huyo ambaye ni muhimu kwenye kikosi cha Yanga wanapaswa kupambana kuvuna pointi tatu.

“Kila mchezaji anaumuhimu wake kwenye kikosi, hatupaswi kutegemea uwepo wa mchezaji mmoja, ni lazima tupambane kama timu kupata ushindi,” alisema Lwandamina.

Alisema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao wa kesho kwa kuwa na wao wamejiandaa na wamejipanga kushinda.

“Mchezo utakuwa mgumu, kwa sababu hata wao (Mbeya City) wamejiandaa, lakini kama wenyeji ni lazima tupambane ili tufanikiwe kupata pointi tatu,” alisema Lwandamina.

Aidha, amesema kutokana na matarajio ya ugumu wa mchezo huo, amewataka wachezaji wake kutumia vizuri kila nafasi watakayoipata kwenye mchezo huo.

Msimu huu Yanga imeonekana kupoteza makali yake ya upachikaji mabao baada ya kushuhudiwa kwenye michezo tisa iliyocheza kwenye ligi imefunga mabao 11 na kuruhusu kufungwa mabao manne huku ikiwa imejikusanyia pointi 17 na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad