Lui Adata na Papa wa Gigy Money

Lui Adata na Papa wa Gigy Money
Baada ya kufanya vizuri katika cover ya ngoma ya Patoranking na Diamond ‘Love You Die’, Msanii Lui ametaja ngoma nyingine ya Bongo Flava ambayo angetamani kufanya cover yake.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘1 on 1’ ameitaja ngoma ya Gigy Money ‘Papa’ kama ngoma ambayo ingeweza kufanya hivyo endapo muda ungeruhusu.

“Ni wimbo wa Gigy Money, ni wimbo ambao kila sehemu ninapoenda naukuta, ukienda club watu wanarudika, ukianza tu haulizi unaruka, kajitaidi sana ingawa sasa hivi muda wake umepita kidogo lakini hadi sasa hivi ni ya moto lakini siwezi kuifanyia tena cover” Lui ameiambia Bongo5.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad