Kwa mara ya pili katika chini ya kipindi cha miezi mitatu, macho yote sasa yanaangazia mahakama ya upeo wa juu zaidi Kenya, itakayoamua iwapo ushindi wa rais Kenyatta, ni halali au la.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Kenya na tume ya Uchaguzi IEBC, baada ya uchaguzi wa marudio ya Oktoba 26.
Kesi tatu zimewasilishwa mbele ya majaji 6 wanaoongozwa na jaji mkuu David Maraga, mbili zikitaka ushindi wa rais Kenyatta ubatilishwe, huku moja ikitaka viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga wachukuliwe hatua kwa madai ya kuchochea wafuasi wao kususia uchaguzi, na kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.
Kesi za kubatilisha ushindi wa rais Kenyatta zimewasilishwa kwa misingi kwamba tume ya uchaguzi ilikosa kuagiza uteuzi mpya wa chama ufanyike baada ya mahakama ya upeo wa juu zaidi kufutilia mbali ushindi wa rais Kenyatta mwezi Agosti.
Mahakama ina chini ya siku saba kusikiliza na kuamua kesi hizo tatu.
Kiongozi wa upinzani nchini humo alisusia uchaguzi huo
Image caption
Kiongozi wa upinzani nchini humo alisusia uchaguzi huo