Mahakama Yatupilia Mbali Kesi ya Diamond, Hamissa Mobetto

Mahakama Yatupilia Mbali Kesi ya Diamond, Hamissa Mobetto
Mwanamitindo Hamisa Mobeto amekwaa kisiki mbele ya Diamond Platnumz baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto kutupilia mbali kesi aliyofunguliwa mwanamuziki huyo juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.
Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Novemba 10 ,2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.
Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi.  Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.
Mobeto  anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.
Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto  anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto  akidai  gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni  kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwa taarifa yenu washapatana na hii kesi Domo kafanya kusudi ili wambea wasistuke na bi masumbuko asijue. ila mahaba ya Hamisa na Dai ni motooooo! tena yasiri kuliko mwanzo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama ni siri kuliko mwanzo sasa wewe ulijua vipi wakati ni siri?

      Delete
  2. Dai na Hamisa wamerudiana kitambo, hayo yoote wameyapanga na mawakili wao. msifiri majuha kama Lednjaa na Halima mapengo.

    ReplyDelete
  3. Anonymous 21:21 inaonyesha ni mtu wa shari hapendi kuona watu wako na raha zao ogopa alie kuumba wacha rohi ya kutu daimond hajao bado so akijisikia kuwa na yeyote he will kama ni huyu bi majaaliwa bi masumbuko hapendi asepe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad