Mahakama Yawahukumu Miaka Wiwili Jera Wafanyabiashara Baada ya Kukamatwa na Madini ya Milioni 500

Mahakama Yawahukumu Miaka Wiwili Jera Baada ya Kukamatwa na Madini ya Milioni 500
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetoa hukumu kwa Wafanyabiashara watatu waliokamatwa na madini ya dhahabu yenye thamani ya shilingi milioni 507 ambayo walikamatwa wakitaka kuyasafirisha bila kibali kwenda nje ya Tanzania.

Mahakama imewahukumu Wafanyabiashara hao miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh.milioni 9 (milioni 3 kila mmoja) baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili kila mmoja.

Katika hukumu hiyo, Mahakama pia imeyataifisha madini hayo yenye uzito wa Kilo 6.242 kuwa mali ya Serikali. ambapo waliohukumiwa ni Mashaka Lucas, Jafarri Hussein na Akifu Mohamed.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema hukumu hiyo imezingatia kuwa Washtakiwa ni wakosaji wa kwanza na wamekiri makosa yao.

“Kwa kuwa ni wakosaji wa kwanza, Mahakama inawahukumu kulipa faini ya Tsh.milioni 1.5 kwa kila kosa na kwa kila mshtakiwa, endapo mkishindwa basi mtapaswa kutumikia adhabu ya miaka 2 jela“
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad