Waziri ametoa tamko hilo jana jioni kwenye kikao cha baraza la mawaziri kilichofanyika Dodoma, ambapo amewaasa mawaziri kujidhirisha na bajeti pamoja na sera za serikali kabla ya kutoa tamko ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza endapo tamko halitatekelezeka.
Mbali na hilo waziri mkuu amewataka viongozi hao wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya uongozi ili kuithibitishia jamii kuwa Rais Dkt. John Magufuli aliwateua kutokana na uadilifu na uwezo wao kiutendaji.
“Tunao wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anafanya kazi kwa nguvu na bidii ili kutimiza matarajio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na wananchi wote kwa ujumla,” amesema waziri mkuu.
Aidha waziri mkuu amewataka mawaziri wafanye ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.