Wakati Emmerson Mnangagwa alipofutwa kazi wiki mbili zilizopita hakuwa makamu wa rais wa pekee nchini Zimbabwe
Phelekezela Mphoko ni makamu wa rais mwengine ambaye anajulikana kwa kumuunga mkono mkewe rais Mugabe na kulingana na sheria anapaswa kumrithi Mugabe.
Hatahivyo chama cha Zanu PF kimsema kuwa Mnangagwa ataapishwa kufuatia uamuzi uliochukuliwa na kamati yake kuu siku ya Jumapili.
Bwana Mphoko alikuwa ameondoka katika taifa hilo wakati Jeshi lilipochukua mamlaka wiki moja iliopita, na kulingana na gazeti la NewsDay hajarudi nyumbani kwa kuwa anahofia kukamatwa.
Gazeti hilo limenukuu duru akisema kuwa amebadilisha mipango yake ya usafiri.
Alitarajiwa kurudi nchini zimbabwe kufikia siku ya Ijumaa , kutoka Tokyo Japan.
Lakini duru zimesema kuwa anataka tiketi zake za usafiri kubadilishwa ili aelekee Zambia au Msumbiji .
Anajua anaogopa kukamatwa kwa sababu anatakikana kwa kuzuia haki na kufanya ufisadi.