Mkuu Wa Mkoa Wa Dar Es Salaam Paul Makonda ameipokea meli kubwa toka China iliyofika kwa ajil ya kuanza zoezi la utoaji wa huduma ya vipimo vya afya pamoja na matibabu ambayo yatatolewa bure kabisa kwa muda wa siku tano.
Ambapo Rc makonda ametoa wito kwa wakazi wote wanaoishi Dar es salaam kuanza kujitokeza kwa wingi kuanzia leo ili waweze kupewa huduma ya vipimo pamoja na matibabu bure hasa kwa wale wenye matatizo mbalimbali.
Aidha ameongeza kuwa anaushukuru ubalozi wa china hasa kwa kitendo cha wao kuruhusu meli hiyo itoe huduma katika nchi ya Tanzania hususan Dar es salaam kwan hiyo inaonyesha kuwa nchi ya china inaunga mkono hasa katika jitihada za Rais Maguful Za Kumtetea Mtanzania Wa Kipato Cha Chini Na Kuhakikisha Kuwa Wanapata Huduma Zote Muhimu.
Meli hiyo ambayo imepokelewa siku ya jana imekuja na madaktari pamoja na wahudumu wapatao zaid ya 381,huku madaktari 30 kati yao siku ya jana tayari wamekwisha fanya ziara ya kuitembelea hospital ya Muhimbili,Amana,Mwananyamala pamoja na Hospital ya Temeke kwa ajili ya kukagua vifaa ambayo vitakuwa vimepoteza umakini wake wa kutoa huduma na kabla ya kuondoka watakabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajil ya hospital hizo. Angalia picha.