Mama Ashura Amshambulia Mwanamuziki Ali Kiba Kwa Show Mbaya Aliyofanya Fiesta

Mama Ashura awapuuza Team Kiba kwa kumshambulia na kuendelea kula sahani moja na Alikiba kwa kumrushia dongo hili kuhusu show yake Kwenye Fiesta Dar 2017. Amesema
.
"Unajua uimbaji wa muziki sio tu ufundi wa sauti, maana kuna ambao wanadhani kwa sababu wanaufundi wa sauti basi muziki wa bongo wameshawini. Big NOO! tambua namna ya kucheza nayo sauti yako na linganisha na mahitaji ya muziki wako, napendaga kumtolea mifano Mondi sio kwamba ndo pekee anayeweza au anayefanya vizuri laa Bali ni mmoja wapo kati ya mifano ya kuigwa. Kipindi anatoka watu wakasema ooh hawezi kuimba anaunga unga vocal yake haina ufundi, lakini sasa hivi ule muono umebadilika baada ya wakimataifa kuuona uwezo wake wa kucheza na sauti yake ambayo ilisemwa ni yakuunga unga kiujanja ujanja. Wapo wengi wenye sauti nzuri na wanajua kucheza nazo mfano mwingine Barnaba na wengine.

SASA wale wakali wa masauti sipati picha wanavyojikakamua kuimba 'Hallelujah' kwa kutumia ufundi wao wa hali ya juu... Matokeo yake ndo hayo kwenye hii video.

Next post nitaongelea show lakini jamani mapovu yapungue looh kwani kutoa maoni dhambi? Na mbona kila mtu aliyekuwepo Fiesta alijionea kwa macho kilichotokea??

.
Nini maoni yako Mdau?? Mama Ashura kasema kweli au ni muongo hana lolote ?

FUNGUKA HAPA

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wewe mama ashura kwanza jitambue wewe ni kichekesho unatafuta kiki kwa nguvu ur such an .....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad