Mama mzazi wa Irene Uwoya, Naima Uwoya, usiku wa kuamkia jana amekesha akimuombea aliyekuwa mkwewe Hamad Ndikumana katika Kanisa Katoliki Mbezi Jogoo, Dar es Salaam. Aidha Mama Uwoya akizungumza na chombo Kimoja cha habari amesema hakuwahi kuwa na tatizo na Ndikumana walikuwa Kama Mama na mwanae.Mama Uwoya amesema kipindi cha nyuma aliwahi kwenda nchini Israel na kufunga kwa Siku kadhaa ili Irene na Ndikumana warudiane lakini haikuwa bahati wao kuwa pamoja tena.
.
Akizungumza huku akilia kwa kwikwi kwa uchungu Mama Uwoya amesema
.
“Ndikumana mimi sijui nianzie wapi, alikuwa mkwe wangu kipenzi alikuwa kama rafiki, alivuka hata ukwe, Ndikumana mkwe wangu siku zote tumeishi nae vizuri, siku zote tumekuwa tukiwasiliana mpaka mwishoni hapa nilikuwa natoka safari, ananiambia mama naomba tuwe na moyo wa subira, mimi nitavumilia yote ya dunia lakini mimi ni mwanao mpaka naingia kaburini, na kweli mpaka anaingia kaburini, mwanangu mimi nilikuwa nampenda” alisikika mama yake Irene Uwoya ambaye alikuwa akilia kwa uchungu.
.
Akizungumza na Mtanzania alisema
.
“Sitaacha kumuombea marehemu mkwe wangu hadi siku naingia kaburini, nitaomba sana ili apumzike kwa amani hata kama ana kinyongo na familia yangu, tulimpenda familia nzima na naamini hata vizazi vyetu vijavyo vitampenda kwa kusikia matendo yake,” alisema mama Uwoya.
.
Alisema atahakikisha anampa faraja mzazi mwenziye (mama Ndikumana), kwa kuongea naye mara kwa mara kama alivyokuwa akiongea na marehemu na kumpelekea mjukuu wake ili amzoee na wajisike faraja ya kumuona mwanaye kupitia Krish.