DILI LA MIL. 400 LA WEMA
Ilifahamika kuwa, dili hilo lilikuwa liende kwa Wema Isaac Sepetu ambaye miezi kadhaa aliripotiwa na gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda kuwa alikuwa amelamba shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuandaa tamthiliya hiyo.
Ilidaiwa kwamba, baada ya sakata la Uwoya na Dogo Janja likishika kasi ndipo kukaibuka ubuyu kwamba, dili hilo aliporwa Wema la sivyo ndiye angeolewa na Dogo Janja ndani ya tamthiliya hiyo.
“Wema alihakikishiwa kabisa kushikishwa shilingi milioni 400 na akaanza kufanya usaili wa mastaa zaidi ya hamsini atakaowatumia na kuwaahidi kuwalipa dau nono.
UWOYA ANUKA FEDHA
“Lakini ghafla ilidaiwa kwamba, Uwoya alifanya ‘umafia’ ndipo dili likahama kwa Wema na kutua mikononi mwake kisha kukamata huo mkwanja na sasa ananuka fedha maana zimemtembelea bidada.
“Ilikuwa rahisi kushinda tenda hiyo maana wakati Wema anataka ashikishwe shilingi milioni 400, yeye alidaiwa kukubali kufanya kazi hiyo kwa shilingi milioni 200 na ushee.
“Unaambiwa sasa hivi bifu la Uwoya na Wema linafukuta na ukizingatia kwamba huwa hawaivi chungu kimoja.
“Nakwambia inasubiriwa siku watakutana uso kwa uso watu waone itakuwaje maana hawajaonana tangu kutokea
kwa ishu hiyo.
“Unaambiwa Wema ana hasira maana tonge lilimponyoka mdomoni hivyo Team Wema wanamuomba Uwoya akae mbali nao,” kilimaliza kumwaga ubuyu chanzo na kulipisha Amani liwatafute wahusika.
MDHULUMIWA WEMA
Jitihada za kumpata Wema ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, lakini alipotafutwa Neema Ndepanya ambaye ni prodyuza na mwandishi wa miswada wa Wema alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli Wema alikuwa na dili kama hilo lakini siwezi kusema ndilo hilo unalolizungumzia (la Uwoya).”
UWOYA ASHTUKA
Alipotafuta Uwoya na kuulizwa juu ya kupora dili la Wema alishtuka na kudai kwamba, ndiyo kwanza anasikia ishu hiyo kutoka kwa mwandishi wetu.
“He! Ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako (mwandishi) na sina maoni juu ya hilo maana sielewi chochote.”
Chanzo: Global Publishers