Mapya Yaibuka Sakata la Kujiudhuru Nyarandu Ofisi ya Bunge Yatoboa Siri

Mapya Yaibuka Sakata la Kujiudhuru Nyarandu Ofisi ya Bunge Yatoboa Siri
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi, CCM, Lazaro Nyalandu  ya kumtaarifu Spika kuhusu uamuzi wake wa kujiuzulu Ubunge.

Taarifa ya ofisi hiyo hata hivyo imesema, Spika amepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu, Bw, Nyalandu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi.
Imeongeza kuwa, CCM kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mh. Spika kuwa, Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho.
Taarifa hiyo imefafanua kwamba, kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi ambacho Lazaro Nyalandu alipata Ubunge kupitia Chama hicho na kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1) (f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba ndugu Lazaro Nyalandu si Mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa.
“Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake cha Ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo, Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama cha chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.” Imesema taarifa ya Spika
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu aliutangazia umma hivi karibuni kuwa anakihama chama hicho na kuonyesha nia ya kuhamia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwa madai ya kuwa chama cha CCM kimepoteza muelekeo.


Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kina Nyalandi Na waliokuwa Kama hai mafisadi Ni watanyooka Tu.
    Hii Ni awamu ya tano

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad