Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Mashinji amefunguka na kusema kuwa baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa udiwani ambao unatarajiwa kufanyika karibuni katika Kata 48 katika mikoa 18 nchini wamepewa maelekezo kutowatangaza Madiwani CHADEMA wakishinda.
Dkt. Vincent Mashinji amesema hayo leo kupitia mtandao wake wa Twitter na kudai kuwa hiyo itakuwa ni fursa kwao wao CHADEMA kuwaonyesha na kuwafundisha ustaarabu mpya.
"Wasimamizi wa uchaguzi wana maagizo ya kutowatangaza madiwani wa CHADEMA watakao shinda. Hii ni fursa kwetu kuwafundisha ustaarabu mpya. Na imani maneno haya utayakumbuka nikupe mshahara, nyumba na gari halafu umtangaze mpinzani kashinda" alisema Katibu Mkuu wa CHADEMA
Mbali hilo Mashinji amejibu hoja ya Rais ambayo aliitoa akiwa Mwanza kuwa wezi ambao walikuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikimbilia CHADEMA na kudai kuwa watu hao ambao wanatoka CCM na kwenda CHADEMA wameamua kuokoka.
"JPM kusema wapo watu waliokuwa ni wezi katika CCM na kusema saizi watu hao wamekimbilia CHADEMA. Lazima JPM ajue kuwa “Wameamua kuokoka” Alisema Mashinji.
Waache Chadema wakumbatie wezi na mafisadi kwa kisingizio cha kwenda kuokoka kwenye chama chao watanzania si wapumbavu. Sasa tayari wameshaanza kutoa sababu za kunyimwa ushindi hata uchaguzi haujafanyika ni dalili tosha yakuwa Chedema inaelekea kuzimu. Kumbatieni tu hayo matapishi yenu mzidi kunuka watu wakiwamimbia mseme mnaibiwa.Mlichana Lowasa ana Sumae na wengine wengi wakati wakiwa CCM kuwa haikuwa haki watu hao kuendelea kuishi uraiani isipokuwa wawe wamesekwa magerezani lakini leo watu hao ni mashujaa kwa Chadema licha ukweli ni kwamba watu hao ni mafisadi. Kwa CCM hii ya Maghuful Chadema mtasema mnaibiwa mara nyingi tu . Maneno na vitendo ni vitu tofauti kabisa na Maghuful anasema kwa vitendo watanzania wakishuhudia mchana kweupe jinsi mzee wa watu anayohangaika na kujitoa sadaka kuhakikisha watanzania na nchi yao wanaondokana na unyonge wa hali na kuelekea kuishi maisha yaliyo bora. Chadema mtalalama sana tu kuwa hamkutangazwa kuwa washindi kwa hiyo staili yenu ya kukumbatia mafisadi wanaokimbia kutoka CCM.
ReplyDeleteWaache Chadema wakumbatie wezi na mafisadi kwa kisingizio cha kwenda kuokoka kwenye chama chao watanzania si wapumbavu. Sasa tayari wameshaanza kutoa sababu za kunyimwa ushindi hata uchaguzi haujafanyika ni dalili tosha yakuwa Chedema inaelekea kuzimu. Kumbatieni tu hayo matapishi yenu mzidi kunuka watu wakiwakimbia mseme mnaibiwa. Mlimchana Lowasa na Sumae na wengine wengi wakati wakiwa CCM kuwa haikuwa haki watu hao kuendelea kuishi uraiani isipokuwa wawe wamesekwa magerezani lakini leo watu hao ni mashujaa kwa Chadema licha ukweli ni kwamba watu hao ni mafisadi. Kwa CCM hii ya Maghuful Chadema mtasema mnaibiwa mara nyingi tu . Maneno na vitendo ni vitu tofauti kabisa na Maghuful anasema kwa vitendo watanzania wakishuhudia mchana kweupe jinsi mzee wa watu anayohangaika na kujitoa sadaka kuhakikisha watanzania na nchi yao wanaondokana na unyonge wa hali na kuelekea kuishi maisha yaliyo bora. Chadema mtalalama sana tu kuwa hamkutangazwa kuwa washindi kwa hiyo staili yenu ya kukumbatia mafisadi wanaokimbia kutoka CCM.
ReplyDelete