Matusi Yamchosha Wema Sepetu Atamani Kufa .” Kuna muda Natamani Allah Subhannah Anichukue tu"

Wema Atamani Afe .” Kuna muda Natamani Allah Subhannah Anichukue tu... Ya Duniya ni Mengi Sana"
Muigizaji mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amesema kuna muda anatamani Mungu amchukue afe ili aweze kupumzika na mambo ya dunia ambayo yanamnyima raha.

Wema Sepetu ameyasema hayo kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram, akisema ingawa anajua ipo siku atakufa, lakini anatamani ingetokea sasa ili aweze kupumzika na mambo yanayomuumiza nafsi yake ikiwemo kutakanwa bila sababu za msingi kwenye mitandao ya kijamii.
Wema Sepetu amendeelea kusema kuwa kutokana na mambo ambayo anayapitia anatamani hata asingetokea duniani, na kuamua kukaa nje ya mitandao ya kijamii kwa muda.
"Ipo siku nitakufa, hakuna anaeishi milele... Sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndo itakuwa, “Maskini ya Mungu, Dada wa watu alikuwa hivi na vile, Mungu ailaze Roho yake mahali pema...” Kuna muda mwingine huwa natamani Allah Subhannah wata’allah anichukue tu... Ya Duniya ni mengi sana", ameandika Wema Sepetu.
Wema ameendelea kuadniak akisema.." Kuna muda mwingine nakufuru mwenyezi Mungu na kutamani labda hata nisinge exist... Ila acha niendelee kumtegemea yeye... Kila jambo hutokea kwa sababu.... Hili nalo litapita... I think I need a Time Off Social Media... Kwa mara nyingine Tena.... Siwezi jamani".
Licha ya hayo Wema Sepetu hajaweka wazi moja kwa moja ni jambo gani ambalo limemkwaza zaidi, kwani kitendo cha kutukanwa na kusemwa vibaya kwake sio jambo geni.


Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole sana mwaya, ila hebu umshauri na 'shostiako' Mange Kimavi awache kutukana watu bila sababu, hata na wao wanaumia hivyo-hivyo ila ......HATUNYWI-SUMU-HATUJINYONGIIIIII.......CCM MBELE-KWA-MBELE hahahaha

    ReplyDelete
  2. Kimwana usiseme hivyo.
    Nimeshamwambia Haji Manara afanye kweli ila anataka Rizaa ya Hamolapa .
    Sasa uamuzi ni wako.
    Eti walisemaga hate yule mwenyekiti pia nae yuko.
    Usiwakologe sana. Wewev chagua mchezo uishe.
    Mbona bado uko katika Fomu kwa miaka miwili ijayo. Ndiyo Maisha Henyu Henyu. Fulaia Maisha.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad