Mayanga Afanya Mabadiliko Kikosi cha Taifa Stars

 Mayanga Afanya Mabadiliko Kikosi cha Taifa Stars
KUELEKEA mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Benin, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga amefanya mabadiliko kwenye kikosi chake.

Mayanga amefanya mabadiliko hayo kwa kuwaondoa Mzamiru Yassin na Erasto Nyoni, huku nafasi zao zikichukuliwa na Jonas Mkude wa Simba na Mudathir Yahaya. Wachezaji hao wameondolewa kutokana na mchezo uliopita dhidi ya Malawi kuonyeshwa kadi nyekundu.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred LuLUCAS, amesema kikosi hicho kimefanyiwa mabadiliko hayo ya haraka kabla ya kuanza kwa maandalizi yanayotarajiwa kuanza Jumapili hii.

Lucas ameongeza kuwa, wachezaji walioitwa katika kikosi hicho ambao wanacheza nje ya Tanzania, wataungana na timu huko Benin.

“Tumefanya mabadiliko kwa kuwaongeza Jonas Mkude wa Simba na Mudathiri Yahaya kutoka Singida United, hii ni baada ya Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin wote wa Simba kutoruhusiwa katika mchezo huo kutokana na kuwa na adhabu ya kadi nyekundu ambazo walizipata katika mchezo uliopita,” alisema Lucas.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad