Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewataka viongozi wa dini kupaza sauti kukemea maovu ili kuiokoa nchi katika kilio.
Mbowe alisema hayo jana wakati wa ibada ya kumuaga marehemu mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Hai, Looka Mushi iliyofanyika katika Usharika wa Nkwarungo.
“Dunia yetu imejaa uovu, sisi ambao tuko kwenye siasa tunatambua nguvu ya viongozi wa kiroho, kauli yao moja kukemea uovu inatingisha nchi nzima,” alisema Mbowe. “Semeni tunatambua tangu enzi mmekuwa mkikemea maovu na ‘kui-shape’ nchi, msione aibu kuwakemea viongozi waovu.
“Viongozi wa dini msiingize roho ya uoga, mtaiponya nchi, mkikaa kimya nchi itakufa, nchi inateketea, nchi inaangamia viongozi msikae kimya watu wanauawa.
“Itafika kipindi kwa kiburi cha madaraka wataamrisha baba askofu alale rumande kwa mfano, Mungu akunusuru sana Baba Askofu Dk Frederick Shoo atakapoambiwa alale ndani ndiyo utakuwa ukombozi wa Taifa letu Bwana Yesu asifiwe,” alisema Mbowe.
Kwa upande wake, Askofu Shoo alisema viongozi wa dini waache unafiki na waige mwenendo wa Mchungaji Mushi.
“Watumishi wengi ni wanafiki, hivyo waache unafiki na kuwa na rangi mbilimbili muige mwenendo wa mchungaji Mushi,” alisema Dk Shoo.
Askofu mstaafu Erasto Kweka alisema matendo mema yaliyotangauliza neno la Mungu ndiyo silaha ya kweli ya kila binadamu.
Alisema jambo muhimu ni kuishi kwa kuangalia waliofanikiwa katika imani walifanya nini.
“Leo tunamuaga mpendwa wetu, anayesifiwa na kila mmoja kutokana na kutukuka kwa matendo yake mema, tutafakari na kutenda kwa kumpendeza Mungu kama alivyofanya Mchungaji Mushi,” alisema Kweka.
Muhubiri katika ibada hiyo, Mchungaji Lewis Hiza alisema watu wanashangaa kwa nini alikuwa na urafiki na Mchungaji Mushi.
“Jibu ni kuwa wazee wanaozeeka vizuri, huwa na urafiki na vijana ili kuwaachia yaliyo mema na neno alilokuwa akiniambia kila siku nishike neno kwa sababu litaniweka pazuri na litakuwa majibu ya kila swali,” alisema Hiza.
Akisoma wasifu wa marehemu, katibu mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Arthur Shoo alisema Mchungaji Mushi alipata tatizo la mapafu mwaka 2008 na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali.
Alisema mwaka 2014 aliugua na kufanyiwa upasuaji na kutolewa uvimbe tumboni katika Hospitali ya Manipal Bangalore nchini India.
“Pia mwaka huohuo alifanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume. Mwaka 2015 alirudi tena India kwa uchunguzi, alionekana anaendelea vizuri japokuwa aliendelea kusumbuliwa na tatizo la mapafu ambalo mzizi wa tatizo ulianza kwenye ugonjwa wa pafu mpaka alipofariki Ijumaa iliyopita,”alisema Shoo.
Kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upizani Tanzania anashawishi viongozi wa dini kuhubiri siasa katika mahubiri yao? Kipi watakacho kuhubiri kuikosoa serikali ya Maghufuli serikali ambayo inapambana kufa na maovu kuliko hata hao viongozi wa dini kuhakikisha haki inatendeka katika maisha ya mtanzania. Kauli ya Mbowe kwa viongozi wa dini ni sawa na SHETANI IBLISI anaejaribu kuwajaza maovu watumishi wa Mungu katika nyoyo zao ili wamuhasi M/Mungu kufanya kazi za kiroho. Mbowe anajaribu kuwalisha maneno viongozi wa dini kitu ambacho ni hitari kwa usalama na utulivu wa nchi. Kila mtu anajua nini kazi za viongozi wa dini katika jamii na utaratibu gani wanapaswa kutumia wanapoona kuna vitu ambavyo vinaigusa serikali . Mbowe anawashauri viongozi wote wa dini nchini wawe na muelekeo wa Shekh Ponda . Mbowe angependelea kuona viongozi wa dini wakiwashawishi waumini wao ambao ni watanzania wakibaguana kwa misingi ya dini. Haiwezekani kiongozi wa dini aikosowe serikali kwa maelekezo ya chadema bila ya kutotokea mgawinyiko ndani ya waumini . Hapa ndipo unapoona jinsi gani viongozi wa siasa hasa wa upizani wanavyosukuma nguvu zao kuitumbukiza Tanzania katika machafuko. Viongozi wa upizani baada ya kukosa mada halisi ya kuikosoa serikali ya Maghufuli wanalazimisha na kujaribu kupotosha mengi mazuri anayoendelea kuwafanyia watanzania. Maghufuli na serikali yake kama ni Rushwa basi serikali ya Maghufuli ni bingwa wa kupambana nayo barani Africa na pengine Duniani . Kama ni madawa ya kulevya basi serikali ya Maghufuli ni vita endelevu kuhakikisha yanatokomea na wahusika wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Kama ni uwajibikaji serikalni basi hakuna kama serikali ya Maghufuli. Sasa unajiuliza kwa mshangao mkubwa nchi gani ya Tanzania anayodai Mbowe inakufa kama si unafiki? Akisema Chadema inakufa kwa hivyo anaomba msaada kutoka kwa viongozi wa dini tutamuelewa lakini awe makini sana na huko kutapa tapa kwake kwani watanzania wengi tunaunga mkono kauli ya Tanzania kwanza chama baadae na chini ya serikali ya Maghufuli hapana shaka yeyote Tanzania na watu wake inatendewa haki yake yakuwa kitu cha kwanza kuliko mambo ya uchama. HONGERA SANA JEMBE MAGHUFULI MUNGU AKUWEKE.
ReplyDeleteHuyu mbowe anaxhotaka hasa ni nini?
ReplyDeletekama ni kilemba cha ukoka ameshavishwa
kama ni upigaji wa Siav
co.. wakati umeshampita.
kilichobaki ni Malimbikizo ya Kodi. ikiwa tumeqeza ya Lugumi tunangoja ni ya Mbowe
msigwa anazungumzia hilo hilo la viongozi wa Dini
sasa kwa taarifa yako kama hujuibDini.
Dini yetu sisi inatusisitiza kuwa tii viongozi na wale wenye mamlaka juu yetu beside kuwa waadilifu na waaminifu. ila ikiwa tumejiwa kwa shari au kudhulumiwa haki yetu pale ndiyo tunaweza kufanya mengine ikiwa pia usuluhisho umeshindikana.
Mbowe inabidi uzijue Dini na Madunzo yake katika Amani na Kuishi kwa ummoja na Heshma na Upendo.
Kwa Magu na uongozi wake Sote tumeridhika na ni mchapa lazi.
Mungu amlinde na amuepushe na wenze shari na wapika majungu kama wewe.
Ameen yatakushinda Mbowe
Mbowe nasikia tetesi kuwa wanataka kukuvua uenyekiti na uanachama hawa viongozi wapya ajili hawakuelewi.
ReplyDeletelisemwalo lipo na kama halipo.....
sasa nani atakae shika hatamu nasikia pia kile chama kingine pia kiko katika mchakato wa kuona hilo linafaanikiwa.
JIHADHARI NA UWE MWANGALIFU.
HIYO NI TAHADHARI YANGU KWAKO