Mbunge Leonidas Gama Kuzizikwa Leo Kijijini Kwao

Aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama anazikwa leo kijijini kwao Likuyu Fusi wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Ibada ya mazishi imefanyika leo Jumatatu Novemba 27,2017 nyumbani kwao kijijini Likuyu Fusi umbali wa kilomita 25 kutoka Songea mjini. Mazishi hayo yamehudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Gama alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi Novemba 23,2017 katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho alikopelekwa baada ya hali yake kubadilika akiwa nyumbani kwake.

Taarifa ya Bunge iliyotolewa baada ya kifo cha Gama ilisema mbunge huyo alirejea nchini Novemba 11,2017 akitokea India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad