Mbunge Sugu Kweli Sugu Awachana Wabunge wenzake Kisawasawa...Alaani Airport Kujengwa Chato Badala ya Butiama

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amekosoa mpango wa kujengwa kwa Uwanja wa Ndege wilayani Chato mkoani Geita na kusema kwamba hauna faida yoyote kwa Taifa kwani Rais Magufuli akishatoka madarakani hakuna ndege itakayokuwa inakwenda huko.

Akizungumza leo bungeni wakati wa kujadili mipango ya maendeleo ya taifa, Mh. Mbilinyi amesema kwamba suala la kwamba wakikosoa kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato ni kuchukulia kama suala binafsi bali ni suala la Mipango.

"Mipango bila utaratibu haiwezi kuwa mipango, Mh. Mwenyekiti. Namna ambavyo Airport ya Chato ilivyokuja haikuwa na mipango. Mipango kama hii inanikumbusha Rais Mobutu ambaye alijenga Ikulu kijijini kwao kipindi cha utawala wake na sasa hivi Ikulu hiyo imegeuka nyumba ya popo" Mbilinyi.

Mh. Mbilinyi ameongeza.  Tukianza kuongea hivi kuna watuu wanawaka lakini mkumbuke hii siyo 'personal' bali nazungumzia 'Principal'. Mnashindwa kwenda Butiama kwa Baba wa Taifa mtaenda Chato?

Pamoja na hayo Mh. Mbilinyi ameitaka serikali itumie mbinu ya waliyoitumia kwenye kukuza biashara ya Korosho itumie mbu hizo pia kwenye kukuza bei ya mazao mengine nchini kama mbaazi, Tumbaku na mazao mengineyo.

Hata hivyo Mbilinyi amewaasa mawaziri kutoshindana kutoa matamko ambayo wanajua hayawezi kutekelezeka bali watumie nafasi zao katika kumshauri Rais ili kusonga mbele kutekeleza mipango.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad