Meneja Wa Diamond ‘Babu Tale’ Ana Hatihati Ya Kuswekwa Rumande

Meneja wa Diamond, Babu Tale amejikuta katika upande mbaya wa sheria baada ya yeye na ndugu yake Iddi Tale Tale kushindwa kulipa fidia ya shilingi milioni 250 kutoka katika kampuni ya Tip Top kwenda kwa Mhadhiri wa dini ya kiislamu. Sheikh Mbonde juu ya kosa la matumizi ya kanda za mahubiri ya kiislamu kibiashara bila ruhusa.

Mwaka Jana mwezi februari, mahakama kuu kanda ya Dar es salaam iliwataka Babu Tale na Iddi Tale Tale kama Wamiliki wa kampuni ya Tip top walitakiwa wamlipe fidia Sheikh Mbonde fidia ya milioni 250 na juni mwaka huu mahakama iliamuru Wakurugenzi hao waweke wazi thamani za kampuni hiyo na kama watashindwa kutaja mali za kampuni basi wao watalipia fedha hizo au mali zao binafsi kukamatwa na kuuzwa endapo hawatakuwa na fedha za kufidia.

Pia kama hawana mali yoyote basi watakamatwa na kufungwa gerezani kama wafungwa wa kesi ya madai kwa mujibu wa sheria.

Katika hati ya madai ya kesi hiyo namba 185 ya mwaka 2013, Sheikh Mbonde aliingia makubaliano na kampuni hiyo ya kutumia kazi sake za mawaidha kwakuzalisha, kurekodi na kuzisambaza. Vile vile makubaliano mengine yalikuwa kulipia gharama za kurekodi masomo na mafundisho ya mihadhara

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad