Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema matukio yanayoendea nchini yakiwemo yale ya Mkuranga, Kibiti na kupigwa risasi kwa mbunge wa singida Mashariki, Tundu Lissu ni matukio ambayo vyombo vya dola vinaendelea kufanya uchunguzi huku akieleza na uchunguzi huo hauwezi kufanyika kwa siku moja kwasababu wanaotenda matendo hayo wanatumia mbinu nyingi za kujificha hivyo vyombo hivyo vinatakiwa kutumia mbinu za kuwatambua waliotenda.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma katika Mkutano wa 9 kikao cha 3 kinachoendelea baada ya Mbunge wa Kambi rasmi bungeni, Freeman Aikaeli Mbowe kuhoji serikali inachukuwa hatua gani kwa matukio yanayoendelea nchini likiwemo la Mbunge huyo na kupotea kwa msaidizi wake Ben Saanane.
“Nataka nieleze kwamba amani yetu utulivu ndani nchi ni jambo ambalo Watanzania wote tunatakiwa tushikamane katika kulidumisha, ndilo ambalo linaendelea zidi kutupa heshima duniani kwasababu Watanzania wote tunashirikiana katika hili, yapo matukio yanayojitokeza Mh. Mbowe umezungumzia kwa upande wa siasa matukio haya yapo kwa ujumla wake nchini kwenye maeneo kadhaa kwenye ngazi ya familia lakini pia na maeneo mbalimbali ya mkusanyiko na watu pia wengine wako watu ambao hawana nia njema nchini wanajitokeza katika kutenda matendo hayo, na hata hili unalolisema la Mh. Tundu Lissu sio Mh Tundu Lissu pekee ingawa hatupendi mambo kama haya yatokee lakini pia tumepoteza Watanzania wengi unakumbuka wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji tumepoteza watu wengi lakini pia hivi karibuni Kamanda wetu wa Jeshi la ulinzi nchini JWTZ nae alipigwa risasi pia kwa hiyo tuyazungumze haya kwa ujumla wake na tunapoyazungumza haya kwa utamaduni tulioujenga wa nchi hii katika kujilinda wenyewe kuhakikisha nchi hii inaendelea kuwa salama nataka nikuhakikishie kwamba vyombo vyetu vya dola vinaendelea kufanya uchunguzi wa haya na uchunguzi huu hauwezi leoleo ukapata ufunguzi kwasababu wanaotenda matendo haya wanatumia mbinu nyingi kujificha na sisi lazima tutumie mbinu za kutambua hao waliotenda matendo hayo katika kila eneo ili baadae tuweze kutoa taarifa ya jibu,” amesema Majaliwa.
“Nataka nikuhakikishie kuwa vyombo vya dola haviko kimya vinaendelea, nataka nikuhakikishie vilevile vyombo vya dola vina uwezo wa kusimamia usalama ndani ya nchi, ni suala la muda na ni muda gani wana kamilisha utaratibu hatua gani zichukuliwe sasa hilo linategemea na waliotenda matukio na ni namna gani wamejificha, na sisi tunatumia njia mbalimbali kuweza kuyapata haya na kuweza kujua na kutoa taarifa kwa Watanzania nataka nikusihi na familia zote ambazo zimepata athari ambao wameripoti polisi na vyombo vya dola vinaendelea kwamba pale tutakapo kamilisha uchunguzi tutatoa taarifa kwa ngazi za familia ambazo zimepata athari au ndugu, jamaa waliopata athari hiyo na kuwaambia hatua ambayo sisi tunachukua ,” ameongeza Waziri Majaliwa.
Hivi vichwa vya *Habari mbona vya kushabiki
ReplyDelete