Mh. Zitto Kabwe Aachiwa, Polisi Wachukua simu yake

Kiongozi wa Chama chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe ameripoti kituo cha polisi kilichopo Kamata Karikakoo jijini Dar es salaam kama alivyotakiwa na jeshi hilo. Jeshi hilo limechukua simu ya Mh. Zitto kwa maelezo kuwa itasaidia uchunguzi wao.

Katibu – Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Ado Shaibu amesema kuwa baada ya kuichukua simu hiyo wameahidi watairudisha kwake kesho jioni huku akitakiwa kuripoti kituoni hapo Novemba 27 mwaka huu.

Pia ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa litakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT – Wazalendo, kwa Lengo la kufanya upekuzi wa Ofisi hizo wakitafuta nyaraka zilizotumika na Chama kufanya uchambuzi wa takwimu za Serikali ambao unaonyesha uchumi wa nchi yetu unasinyaa.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu Kilaza hayo yote hana Weledi nayo.
    hivyo alikwendaga Shule??
    Wapi??

    ReplyDelete
  2. Huyu Kilaza hayo yote hana Weledi nayo.
    hivyo alikwendaga Shule??
    Wapi??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad