Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni

Kambi rasmi ya upinzani bungeni imelaani na kupinga vitendo viovu alivyotendewa Mnadhimu wa Kambi hiyo, Tundu Lissu, ambaye alinusurika kifo baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 7, mwaka huu mjini Dodoma

Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, anaendelea kupatiwa matibabu katika   hospitali moja ya Nairobi,   Kenya.

Akiwasilisha bungeni maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni jana kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/2019 kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa kambi hiyo,  Halima Mdee, David Silinde alisema vitendo hivyo vinatakiwa vikemewe kwa uzito unaostahili.

Silinde  ambaye ni Mbunge wa Momba (Chadema), alisema vitendo hivyo vikiachwa viendelee bila kukemewa kuna hatari ya kundi linalohisi kuonewa likakosa uvumulivu na hivyo kuathiri amani ya nchi.

“Ingawa  miezi miwili sasa imepita tangu Lissu anusurike kifo baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi wakati mkutano  wa nane wa bunge ukiwa unaendelea na vikao vyake hapa Dodoma na mpaka sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na serikali juu ya kukamatwa kwa watu waliohusika na tukio hilo.

“Ikiwa polisi wameshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata wahalifu hao ndani ya miezi miwili, Kambi Rasmi ya upinzani bungeni  haioni muujiza wowote unaoeweza kutendeka ili watu hao wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria hata kama polisi wataongezewa miezi mingine miwili.

“Tafsiri ya ukimya huo wa serikali ni rahisi, kwamba hakuna dhamira ya dhati wala utayari wa kushughulikia jambo hilo. Hili la kuanza kutuwinda kwa lengo la kutuua, hatuwezi kamwe kulinyamazia,” alisema.

Alisema Kambi Rasmi ya Upinzani inatoa wito kwa wananchi wote kupaza sauti zao kupinga uonevu na ukandamizaji wa haki, kupinga matukio ya utekaji, utesaji na umwagaji wa damu katika nchi.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivyo Bungeni hamna kazi nyingine za kuleta maendwleo na ubunifu wa kumrahisishia Mtamzamia maisha yake ya kila siku.
    kama ni Lissu ni mmoja latika mamiliomi ua watanzania na ni mbunge wa jimbo kama alivyo KINGWENDU CAha zaidi hasa ni kipi?
    Shighulikieni mambo ya maana na siyo igawanishaji na uchochezi kwa Imma.
    TANZANIA NI YETU NA SISI MDIYO TUTAKAO I JENGA. MIMI NA WEWE.
    LISSU UNAMUOMBEA MUNGU NA UNAANHALIA USTAARABU MWINGINE WA MAENDELEO.
    BUNGENI SI MAHALI PA UPUUZI UPUUZI KAMA HAMUELEWI.
    BUNGE LINA HESHIMA YAKE NA ANAE INGIA NA KUOTWA MP BASI HUYO NI MWWNYE KUJIHESHIMU NA ANAHESHIMU NA ANAFOCUS.
    SIYO KUINGIA KIBAHATI BAHATI KWA AJILI SISI WAPIGA KURA HATUKUIELEWA MAANA YA KURA YETU.
    NAOMBA ELIMU KWA MPIGA KURA IZIDISHQE TOKA NGAi za mitaa / kata/ tarafa na miji ili tuondokane na hawa Vilaza Bungeni.

    Mungu libariki bunge letu na mungu ibariki nvhi yetu utupe AMANI NA USALAMA. NA UMLINDE BABA JPJM..AMEN

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad