Mke wa Mtu na Mchepuko Wake Wakutwa Wamekufa Kwenye Gari Wakiwa Wanafanya Mapenzi

Mke wa Mtu na Mchepuko Wake Wakutwa Wamekufa Kwenye Gari Wakiwa Wanafanya Mapenzi
Mwili wa mwanamke mmoja aliyeripotiwa kuwa ni mke wa mtu mwenye watoto wanne umekutwa kwenye taxi mjini Lagos, nchini Nigeria ukiwa juu ya kifua cha mwanaume ambaye nae alikuwa ameshakufa. Wote wawili wakiwa wamelaliana wakishiriki tendo la ndoa.


Gari lililokutwa kwenye eneo la tukio

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililotokea jumapili ya wikiendi iliyopita wamesema walikuta gari dogo (Taxi) ikiwa imepaki na ndani kukiwa na watu waliokuwa uchi wakiwa wamelaliana ndipo wakaamua kuchukua uamuzi wa kufungua milango.

Shuhuda mmoja alikiri wazi kumfahamu mama huyo na kudai kuwa ameolewa na ana watoto wanne huku akishindwa kumtambua mwanamme aliyekuwa naye.

Baadhi ya maelezo ya mashuhuda kupitia mitandao ya kijamii wamesema walikuta gari na AC ikiwa imewashwa.

Hata hivyo hakuna taarifa rasmi kutoka jeshi la polisi nchini humo kuhusu tukio hilo la kusikitisha.Pitia baadhi ya tweets za mashuhuda wa tukio hilo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad