Mkude Ajiandaa Kubeba Virago Simba

Mkude Ajiandaa Kubeba Virago Simba
KUFUATIA kauli ya mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage aliyesema Jonas Mkude anapaswa kucheza TP Mazembe au Raja Casablanca ya Morocco, kiungo huyo amesema sasa anaanza kujiandaa kuondoka klabuni hapo.
Rage mapema wiki hii, aliliambia gazeti hili kwamba, Mkude ana kiwango kikubwa hivyo anapaswa kuchezea moja kati ya timu kubwa za Afrika hata TP Mazembe ya DR Congo au Raja Casablanca.
Alisema Mkude ni mmoja wa wachezaji wenye uwezo Simba ambaye amekuwa akimtabiria kufika mbali zaidi iwapo atajituma zaidi ili kuweza kucheza nje.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkude alisema kauli hiyo ya Rage imemzindua na sasa anapambana kufa na kupona aweze kupata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.
“Rage alikuwa mwenyekiti wangu kwa muda wa miaka minne, hivyo ananifahamu vizuri kiwango changu, tena zaidi ya sana, tangu alipokuwa akiongoza.
“Amenipa hamasa kubwa ya kuweza kujituma na kupambana niweze kufanya vizuri kwa ajili yangu, familia yangu na kwake pia, nimeupokea ushauri wake kwa mikono miwili na ninashukuru kwa kunikumbusha.
“Ninajituma zaidi ikiwa ni sehemu ya kujiandaa kuondoka Simba kwenda nje ya nchi kucheza soka la kulipwa na naamini nitatimiza ndoto zangu hizi, naomba Mungu anisaidie,” alisema Mkude.
Mwanzoni mwa msimu huu, Mkude alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba baada ya ule wa awali kuisha.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mkude hayo maneno ya Rage wala yasimvimbishe kichwa. Kwa kuangalia kwa haraka Tanzania hakuna club yenye baraka kama Simba kwa nchezaji mwenye kujitakia maendeleo yakwenda kucheza nje ya Tanzania sema vijana au wachezaji wetu ni wazembe. Yeye Mkude mwenyewe ndie aliejicheleweshea maendeleo. Kama ameamka na kundua kuwa ameshachelewa basi asisubiri kujiremba na aanze safari kwa bahati Simba inashiriki mashindano ya kimataifa na aonyeshe uwezo wake huko kwani ndiko atakapoonekana na kina mazembe nakadhalika.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad