‘Mpemba wa Magufuli’ Kupelekwa Mahakama ya Mafisadi

‘Mpemba wa Magufuli’ kupelekwa Mahakama ya Mafisadi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo November 1, 2017 imeelezwa kuwa jalada la kesi ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo ya Tsh. Milioni 785 inayomkabili Mfanyabiashara Yusuf Ali maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli’ linaandaliwa kupelekwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kwenye ‘Mahakama ya Mafisadi’

Haya yameelezwa na Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo ulishakamilika na kinachofanyika sasa ni jalada la kesi hiyo kuandaliwa ili liende Mahakama ya Mafisadi.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi November 15, 2017 ambapo katika kesi hiyo mbali ya Mpemba, Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh 785.6 milioni.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na October, 2015 wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za Serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo 50 vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh 392.8 milioni bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

October 26, 2015 Washtakiwa hao wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande vya meno ya tembo 10 vyenye uzito wa kilo 13.85 vya thamani ya dola za Marekani 30,000 sawa na Sh 65.4milioni.

Wanadaiwa kuwa October 27, 2015 wakiwa Tabata Kisukuru pia walikutwa na vipande vinne vya meno hayo ya tembo yenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya dola za Marekani 15,000 sawa na Sh  32.7 milioni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad