Mpira wa Adhabu ‘Free-Kick’ ya Ashley Young Yamchanganya Mourinho

‘Free-Kick’ ya Ashley Young Yamchanganya Mourinho
Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho ameeleza namna alivyochanganyikiwa na mpira wa adhabu “free-kick” uliyoenda kupigwa na winga wake, Ashley Young katika mchezo wao wa hapo jana usiku dhidi ya Watford.

Mourinho alishtushwa kwa kitendo cha winga huyo kupiga mpira huo uliyokuwa umbali wa mita 30 ilihali si miongoni mwa wachezaji wazuri waliyopangwa kupiga mipira ya haina hiyo.

Wakati wa kwenda kupigwa kwa mpira huo meneja huyo wa United alionekana kuchanganyikiwa kupitia kamera zilizokuwa zikionyesha mchezo huo.

“Nilishitushwa na kitendo cha Paul kumpatia nafasi ile ya kupiga mpira.” Amesema  Mourinho.

“Sikushangazwa na shuti lake bali kupata ile nafasi ya kupiga mpira hakika yupo vizuri na kiwango chake kinaridhisha katika mazoezi kwahio tunafahamu ataendelea kufunga lakini Paul pia amefanya vizuri.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad