Makamu wa zamani wa rais wa Zimbabwe, ambaye kufutwa kwake kazi kulisababisha kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, anatarajiwa nchiuni humo siku ya Jumatano.
KIongozi huyo baadaye anatarajiwa kuapishwa rasmi Ijumaa, kulingana na shirika la utangazaji la Zimbabwe (ZBC).
Emmerson Mnangagwa, aliyetorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo Jumatano nchini , kulingana na Zanu-PF.
Kuondoshwa kwake madarakani kulisababisha chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala wa miaka 37 wa Bwana Mugabe.
Taarifa kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amejiuzulu zilikuja kwa njia ya barua iliyosomwa bungeni Jumanne , bunge likalazimika kuahirisha mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa dhidi yake.
Taarifa hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane