Mswada wa Kuanzisha Chombo cha Kudhibiti Sekta ya Usafiri Majini Kupelekwa Bungeni

Mswada Kuanzisha Chombo cha Kudhibiti Sekta ya Usafiri Majini Kupelekwa Bungeni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa  amesema serikali ya Tanzania imedhamiria kuanzisha chombo cha kuendesha na kudhibiti sekta ya usafiri majini.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo wakati akijibu hoja ya Serikali kuhusu Muswada wa sheria ya wakala wa meli wa taifa mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu jijini Dodoma.
Prof. Mbarawa amesema serikali ipo kwenye mchakato wa kupeleka Muswada bungeni ili itungwe sheria ambayo itaanzisha Shirika  la Wakala wa Meli wa Taifa (NASAC)  ambalo litasimamia usalama wa meli na bahari kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa bandari.
“Tumeandaa Muswada kwaajili ya kuundwa kwa Shirika  la Wakala wa Meli wa Taifa (NASAC) ili kusimamia meli na bandari zetu kama mnavyojua bandarini kumekuwa na changamoto nyingi ambapo hivi karibuni tumeshuhudia upotevu wa mali na vitu vingi pale bandarini kama vile madini na vitu vingine vinaingia bila utaratibu,” amesema Prof. Mbarawa.
Aidha waziri Jafo ameongeza kuwa Serikali imeona ni vizuri ibadilishe mtazamo uliokuwepo zamani kupitia SUMATRA ambayo inasimamia masuala ya nchi kavu na majini na sasa ni vyema kuongeza chombo kingine kwaajili ya kuboresha zaidi utendaji kazi na usalama.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad