Mtazamo Wangu wa Show ya Fiesta Usiku wa Kuamkia Leo...Waliofanya Vizuri na Waliochemsha


Mtazamo Wangu wa Show ya Fiesta Usiku wa Kuamkia Leo...Waliofanya Vizuri na Waliochemsha

MCHAMBUZI BLOG / moments ago



Usiku wa kuamkia leo pale leaders kulikuwa na kilele cha Fiesta huku waandaaji wakijipambanua na kauli mbiu ya 100% local, yaani wasanii wote watumbuizaji wanatoka nyumbani.

Watazamaji
Watazamaji kiukweli walijitokeza wengi hasa ukizingatia kiingilio kilikuwa sh
10000 na promo iliyofanyika watu hawakusita kwenda

Watumbuizaji/ wasanii

Wasanii walijitaidi kuvaa vizuri kwa namna ambayo waliona watandeza.

Jukwaani

Waandaaji walijitaidi kuwawezesha wasanii waimbe live band na hapa ndo tatizo kubwa lilipotokea
Wasanii wengi hawajui kuimba live band huku wakijiconnect na mashabiki hili lilisababisha show kupooza hakukuwa na shangwe

Wasanii wakifika jukwaani wanapiga story nyingi mpaka wanaboa mfano wasanii Jux na Vanessa mdee walitumia muda mwingi kuombana msamaa kuhusu mapenzi yao kuliko kupiga show

Kuchanganya Bongo movies na kuimba jukwaani

Mfano kitendo cha kuwapandisha jukwaani Ebitoke, Mama Ashura na Tausi kulibadilisha maana kutoka tamasha la music hadi kuwa la maigizo zikawa drama nyingi jukwaani hadi zinaboa

Ommy dimpoz kiukweli alizingua sana sijui tatizo hajui kuimba na live banda au alikamia sana kiwango chake kilikuwa chini sana kuliko hata wasanii wachanga

Wasanii waliofanya Vizuri

Rostam- roma na stamini walijitaidi sana kuleta amsha amsha

Rich Mavoko- alijikita zaida kuimba kuimba kuliko kupiga story jukwaani inawezekana kwasababu sio muongeaji sana.

Ben paul- alijitaidi kuwa mbunifu na kuimba vizuri alianza kuaribu alipompandisha ebitoke na kuleta maigizo

Rosa Ree -Katika show alikuwa na Mwanamke Pekee aliyowakilisha wadada katika miondoka ya kuchana au kufoka foka ...Show yake ilivutia

Nyandu toz na mr blue- walipiga show ya maana kuliko hata wale waliokuwa midomoni kwa watu

Jux na vanesa - walijitaidi japo walikuwa wanaboa kwa maongezi mengi jukwaani

Alikiba- alikiamua japo kulikuwa na tatizo la sauti, sijui ni mic yake ilikuwa mbovu au vyombo vya bendi ndo vilikuwa vinazingua, nadhani ndo kilichosababisha asiwe kwenye ubora wake.

Hitimisho

100% local ni wazo zuri la kujenga kujiamini kwa wasanii wetu ila nadhani bado tunapaswa kujifunza kutoka kwa wasanii kama Wizkid, Davido na Patoranking hawa wakiwa wanaimba live.

By Brave one

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huo ni mtazamo wako, haupingiki......wengine tuli-enjoy MWANZO-MWISHO, hasa zile comedy mimi ndio 'ugonjwa' wangu....BIG-UP CMG

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad