Mwakimu Mkuu Avuliwa Madaraka Kwa Kosa la Kubaka Mwanafunzi

Mwakimu Mkuu Avuliwa Madaraka Kwa Kosa la Kubaka Mwanafunzi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Abdalah Malela amemvua madaraka Mwalimu Mkuu Masunga Ng’waya wa Shule ya Msingi Mwashagata, iliyopo kijiji hicho kata ya Ihusi kwa kosa la ukosefu wa maadili.



Akizungumza na mwandishi wa gazeti Habarileo, mkurugenzi huyo alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni la baada ya mwalimu mmoja wa shule yake kumrubuni mwanafunzi wake kwa kufanya mapenzi naye tena kwenye nyumba yake, kitendo ambacho ni cha kukosa maadili.

“Imebainika hili ni tukio la nne kwa mwalimu huyo kutuhumiwa kufanya mapenzi na wanafunzi tofauti tofauti lakini amekuwa hachukuliwi hatua, lakini mimi kwa mujibu wa sheria nimemvua madaraka mwalimu mkuu huyo ili awe mwalimu wa kawaida, sababu amekosa maadili ya kuendelea kushika wadhifa huo,” alisema mkurugenzi huyo.

Aidha, alisema kesi hiyo tayari imefikishwa polisi na wakati wowote mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani. Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga alisikitishwa na kitendo hicho na kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kumchukulia hatua na kuwashauri wazazi wamuache mwanafunzi huyo aendelee na masomo yasije yakampita huku hatua za kisheria kwa mtuhumiwa zikiendelea.

Mlezi wa mwanafunzi huyo, alisema mwanae alisimama masomo kwa muda wa wiki mbili kutokana na tukio hilo. Mwalimu Ng’waya alipozungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu alikiri kuvuliwa madaraka na kueleza amekuwa mwalimu wa kawaida huku akiendelea kufundisha katika shule hiyo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad