Mwasiti Afunguka Kinachomfanya Kuwa Kimya Katika Game

Mwasiti Afunguka Kinachomfanya Kuwa Kimya Katika Game
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Mwasiti ameeleza sababu za ukimya wake katika game kwa kueleza kuwa yupo katika utaratibu wa kukamilisha albamu.
Endapo muimbaji huyo wa ngoma ‘Kaa Nao atafanikiwa kuitoa kwa mwaka huu ataungana na wasanii kama Lady Jaydee, Chege, Ben Pol na Navy Kenzo ambao wameshakwisha kufanya hivyo.

“Nakumbuka last time nilitoa Kaa Nao, nimekaa kimya kidogo lakini nafikiri kimya changu watu huwa wanakiulizia na watu watengemee kazi nzuri kwa sababu najipanga kumalizia albamu pengine nafikiri inanibana sana nakuwa nawaza vitu viwili kwa wakati mmoja” amesema Mwasiti.

“Lakini watu watengemee kazi nzuri kama siyo December nafikiri January mwanzoni na watafurahi kiukweli” ameongeza.

Si Mwasiti pekee yake aliyezungumzia suala la albamu kwa mwaka huu, kuna Fid Q, Izzo Bizness, Diamond, Roma na Stamina (Rostam), Wakazi na wengineo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad