Mwenyekiti wa Kijiji Afukuzwa Kazi kwa Kupiga Chabo

Picha si ya Tukio
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amemsimamisha kazi mwenyekiti wa kijiji cha Sayu, Mataifa Balekele mwenye umri wa miaka 54, kwa kulalamikiwa na wananchi kuwa na tabia ya kuwachungulia kwenye madirisha wakiwa wamelala usiku (Chabo).

Taarifa za mwenyekiti huyo zilifikishwa na wanakijiji kwenye mkutano uliofanyika na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya Bi, Josephine Matiro,alipokuwa kwenye ziara yake, na kumchukulia hatua hiyo ya kumsimamisha kazi huku kukemea vikali akisema ni utovu wa maadili.

Akisimulia tukio hilo Ofisa Mtendaji wa kata hiyo Denis Kimwaga amesema kuwa muhusika alikiri kufanya matukio hayo na alilipishwa faini, huku akidai ni shetani alimpitia.

“Kikao hicho kiliridhia mwenyekiti huyo asimamishwe kazi kutokana na tabia hiyo ya kuchungulia kwenye kaya za watu wakiwa wamelala huku yeye mwenyewe akikiri kufanya vitendo hivyo akidai kuwa amepitiwa tu na shetani na kuomba kuwalipa fedha kama fidia watu aliowachungulia,” amesema Bwana Kimwaga.

Baada ya kumchukulia hatua mwenyekiti huyo, Mkuu wa Wilaya huyo alimteua Paul Selena kukaimu nafasi hiyo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad