Nape Nnauye Ashtushwa na Mapendekezo ya Serikali

Nape Nnauye Ashtushwa na Mapendekezo ya Serikali
Mbunge wa Mtama Mh. Nape Nnauye amedai kwamba ameshtushwa sana na mapendekezo ya serikali kuhusu kuwekeza pesa kwenye miradi ambayo inaweza kuendeshwa kibiashara.

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye
Akichangia leo Bungeni kwenye mjadala wa kujadili Mpango wa Taifa , Mh. Nape amesema kwamba baadhi ya miradi ambayo ingeweza kutekelezwa na sekta binafsi ni ujenzi wa reli ya kisasa ya kati, mradi wa umeme Rufiji, mradi wa bandari na uboreshaji shirika la ndege.
Nape amesema kwamba aliposoma mapendekezo alishtuka baada ya kuona kwamba Serikali inapendekeza kuwekeza pesa za Serikali kwenye miradi ambayo inaweza kuendeshwa kibiashara ambayo pia watu binafsi wangeruhusiwa kuiendesha.
"Kama mpango huu utatekelezwa kama ulivyo, miradi hii inakwenda kuuwa uchumi wa nchi yetu. Miradi hii mikubwa inaweza kujiendesha kibiashara na ikajilipa yenyewe, Niweke rekodi sawa Sipingi kutekelezwa kwa miradi   mikubwa ila napingana na Serikali jinsi ya kuifadhili na kuiendesha kwa kutumia fedha za Serikali" Nape
Akiendelea kusimamia hoja yake Mh. Nape amesema kuwa miradi hiyo ni mikubwa na itagharimu fedha nyingi ambazo zitailazimisha Serikali kukopa fedha nyingi, hali ambayo itaathiri deni la taifa ambalo kwa sasa Dola bilioni 26.
“Serikali ikienda kukopa na kwa sababu miradi hii inachukua muda mrefu maana yake tutaanza kulipa deni kabla ya miradi hiyo haijaanza kurudisha faida kwa taifa. Kwanini tunataka kung’ang’aniza kuchukua pesa ya Serikali”. Hebu tufikirie upya. Dk Mpango rudini mkafikiri upya”  Nape
Nape ameongeza kwamba "Huu mpango wako mzuri lakini rudini kwenye mawazo ya kutumia sekta binafsi. Tukienda hivi tunaenda kuua uchumi,”alisema

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu nape nae ilimradi afungue domo lake hajui hata anachokizungumza. Ubinafsishaji ndio ulioimaliza Tanzania kimaendeleo . Mashirika na miradi mikubwa tu imeangamia Tanzania baada ya kuwachiwa watu binafsi kuiendesha yeye Nape anachokiongea kitu gani? Ni upuuzi mtupu. Kama vile haitoshi ni mpumbavu wa akili pekee kama kiongozi kuishauri serikali kuwaachia watu binafsi kumiliki njia kuu ya Railway yaani hayo ni mawazo pumba kabisa . Hata hizo nchi mabingwa wa ubinafsishaji duniani na Wenye raia wenye uwezo kama Marekani Hawajabinafsisha Reli yao licha ya changa moto tele zinazozikabili mashirika yao ya reli lakini kikubwa na chenye ku make sense ni kuhifadhi wa usalama wa taifa katika kumiliki Njia kuu za usafiri. Leo hii kuna mpuuzi mmoja kaenda kuizuia ndege ya Bombardier kule canada? Na inasemekana huyo mdai aliyoizuia ndege hiyo chanzo chake ni madai magumishi ya ujenzi wa wa barabara. Inawezekana watanzania wenye asilimia zao kwenye hilo deni ndio wafunguzi halisi wa hiyo kesi. Sasa leo mtu anasimama tena kwa kujinasibu kuwa anatoa mawazo smart ati mradi mkubwa wa reli wapewe watu binafsi?kama si ugonjwa wa akili kitu gani?Labda tuje tusubiri yatukute ya Bombardier hakuna barabara, ndege imezuiwa baada ya kutarajiwa kufanyanya biashara sasa na kisha tuje kuwapongeza hao matapeli kwa kuwalipa pesa zaidi .Hata ukifika New York city utaona jinsi gani shirika lao la reli pamoja na njia zake zilivyo taabani licha kupigiwa kelele ya kubinafsishwa serikali ya New York inasema hapana watakufa nalo lakini liwepo chini ya mamlaka ya serikali. Hawa wanaojiita wanasiasa wetu wakati mwengine wachunguzwe akili zao maana wanakwenda kupotosha wananchi kule bungeni.

    ReplyDelete
  2. Yeye Nape anashindwa kufahamu yakwamba nchi kama Tanzania ili uchumi wake uimarike ni lazima serikali ilazimishe kuanzisha uanzishaji wa miradi mikubwa hata kwa pesa za mkopo kwani njia pekee kuu na haraka ya kuzalisha ajira. Hakuna cha kuuwa uchumi hata siku moja katika kuanzisha miradi mikubwa kwami ukweli ni kwamba ni njia moja wapo nzuri kabisa ya kuzalisha ajira na kuamsha mzunguko wa fedha kwa wananchi na kupelekea mchocheo wa uchumi wa taifa

    ReplyDelete
  3. Nape ... Tumeishi na Marehemu Baba yako alikuwa mstaarabu na Hana Domo Kaya.
    Wewe umelipata wapi?
    Kazi nyingine tutakupangia lakini kwa mwelekeo huu na Domo kaya Hili. Inatufanya Turudi nyuma.
    Kama ni Steve na Wema mbona wanakujua Vizuri tu.
    Jifundishe Kula Ganzi.
    Wewe ni Kijana wetu. Nadhani Unanielewa.

    ReplyDelete
  4. Nape ... Tumeishi na Marehemu Baba yako alikuwa mstaarabu na Hana Domo Kaya.
    Wewe umelipata wapi?
    Kazi nyingine tutakupangia lakini kwa mwelekeo huu na Domo kaya Hili. Inatufanya Turudi nyuma.
    Kama ni Steve na Wema mbona wanakujua Vizuri tu.
    Jifundishe Kula Ganzi.
    Wewe ni Kijana wetu. Nadhani Unanielewa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad