Nape Nnauye Atoa Neno Kwa Vyama vya Upinzani Baada ya Uchaguzi wa Madiwani

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, amekiri kuwepo na vitendo ambavyo siyo sahihi ambavyo vilivyojitokeza katika Uchaguzi wa marudio katika baadhi ya kata  na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe.

Nape amefafanua hayo  baada ya kuwepo na malalamiko hayo kutoka upande wa upinzani ambapo amesema  kwamba vitendo hivyo vinapaswa kushughulikiwa kisheria kama wahalifu na siyo kushughulikiwa kisiasa  na kwamba kufanya matendo hayo kisiasa ni njia za kuficha uovu.

Pamoja na hayo Nape ameongeza kwamba hajawahi kuwa muumini wa matumizi ya nguvu kwenye siasa na wala hajawahi kushiriki mipango ya kutumia nguvu bali anaamini katika matumizi zaidi ya nguvu.

Aidha Nape ameongeza kwamba sehemu zote alizofanya kampeni na wala hakubariki matumizi ya nguvu hivyo kuwashauri vyama vya upinzani wafanye tathmini ya kweli kisha kuchukua hatua pale walipoteleza katika uchaguzi.

"Rafiki zangu Upinzani fanyeni tathmini ya kweli halafu chukueni hatua pale mlipoteleza. Hichi kinachoendelea cha kutoa visingizio vya jumla. Sikatai kuwa kulikuwa na baadhi ya maeneo kumekuwa na vitendo si vya kibinadamu  lakini si kwa kata zote. Vitendo hivyo vishughulikiwe specific kisheria kama wahalifu na si kushughulikiwa kisiasa".Amesema Nape

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sikupati vizuri Nape. Sikuelewi. Siasa, ni mfumo, ni mapito tu. Kumbuka wewe u binadamu. Nitasema ukweli daima fitna kwangu mwiko. Kumbuka ulipoumia na ilikuwaje. Naona bado u mwoga. Lakini ni nchi ndiyo iumiayo kwa kutokuwa wakweli, kwa kusema tu bila kuonyesha matendo. Maisha ni kuwa mkweli na kusimamia haki. Wapinzani wanaonewa, wanawekwa ndani. Bado mnatetea chama chenye dhuruma badala ya kutetea haki.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad