Ndege ya Coastal Aviation Yaanguka Ngorongoro Ikiwa na Watu 11

Mapema leo Novemba 15 katika majira ya saa 5 kwa saa za Afrika Mashariki ndege ya Shirika la Ndege la Coastal (Coastal Aviation) yenye namba 5H-EGG, Cessna Grand Caravan ikiwa na abiria 10 na rubani 1 imeanguka eneo la Empakaai wakati ikiwa safarini kuelekea Serengeti.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, hakuna mtu aliyeweza kufika eneo la tukio kujua hali ya ajali hiyo kutokana na kutokea katika eneo ambalo halifikiki kirahisi.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa, timu za huduma za kwanza na mtukio ya dharura wanaendelea na utaratibu wa haraka wa njia ya anga na ardhi kufika eneo hilo ili waweze kutoa msaada.

Coastal wameeleza kuwa mamlaka zote zimepewa taarifa na kwamba wataendelea kuujuza umma wa watanzania kadiri watakavyoendelea kupata taarifa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad