Ndoa ya Kafulila Matatani, Uamuzi wa Mke, Wawashangaza Wengi

Siku chache baada ya aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), David Kafulila kutangaza kukihama chama hicho kwa kile alichokiita… ‘hakuna mabadiliko ya kweli kupitia upinzani…’, imebainika ndoa ya mwanasiasa huyo kijana machachari iko matatani baada ya mkewe kujitokeza hadharani na kuponda vikali uamuzi wake, Risasi Jumamosi linakushushia nondo nzito!
TUANZIE HAPA KWA MKE WA KAFULILA
Baada ya mshangao mkubwa kuzuka miongoni mwa wadau na wakereketwa wa masuala ya kisiasa, siku moja baada ya uamuzi wa Kafulila (Jumatano), mkewe ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Chadema akiwakilisha Mkoa wa Singida, Jesca Kishoa alizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kutoa kauli ambayo wengi waliishangaa.

Kishoa alisema: “Taarifa za Kafulila kuhama chama nimezisikia kupitia vyombo vya habari, nikampigia simu na katika mazungumzo yetu sikuona hoja ya msingi ya yeye kuchukua uamuzi huo, ninavyomfahamu Kafulila ni miongoni mwa watu wenye msimamo na hayumbishwi kirahisi hususan kwenye kupigania ukweli na haki na ndiyo maana mliona jinsi alivyohatarisha maisha yake kwa kuzungumzia suala la Escrow.


“Sasa nimeshangaa sana imekuwaje naye ameingia kwenye mtego wa siasa za kuyumbishwa, huwezi kukemea uovu ukiwa CCM, hilo halipo kabisa na kwa hili nimemshangaa sana Kafulila, kwa upande wangu naona Chadema ndiyo chama kinachofaa kupigania haki na manufaa ya Watanzania, sifikirii kabisa kuhama chama changu.”
MJADALA MZITO
Kufuatia kauli ya Kishoa, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii
walizungumza na mwandishi wetu na kutoa maoni yao juu ya uamuzi wa Kafulila na kauli za mkewe na kubainisha wazi kuwa ndoa ya wawili hao iko matatani na lolote linaweza kutokea endapo watakosa mapatano na misimamo thabiti itokanayo na nguvu za kisiasa.


“Unajua uamuzi wa Kafulila umeelemea kwenye pande mbili, mosi ni binafsi kwamba huo ni uamuzi kwa namna anavyoona na hapaswi kupingwa kwa hatua hiyo, lakini upande wa pili haiwezekani kuchukua uamuzi huo bila kuishirikisha familia kwa maana ya mke au mume tena ukizingatia kwamba wote ni wanasiasa, ukiona hivyo basi kuna tatizo kwenye ndoa hiyo.

“Kafulila amehamia Chadema hivi karibuni, unataka kuniambia kwamba hakumshirikisha mkewe? Siyo rahisi lakini kwa nini sasa hivi ahame chama bila kumdokezea mkewe? Kama amefanya hivyo kwa jambo zito na kubwa kama hilo ni mambo mangapi ambayo mke au mume huyafanya bila kumshirikisha mwenzake, ukitazama kwa mapana sana, ni wazi kwamba ndoa ya Kafulila ‘iko ICU’,” alisema mwanasiasa mmoja mkongwe, ambaye ni wa chama cha upinzani nchini.


“Kauli ya mke wa Kafulila inatoa tafsiri kubwa mno kuhusu ndoa yao. Kwamba hakuna kushauriana, ushirikiano na hakuna heshima. Nasema kushariana kwa sababu amesema taarifa za mumewe kuhama chama amezisikia kwenye vyombo vya habari kama mimi na wewe, pili hakuna kushauriana kama mtu anaamua kufanya jambo la namna hiyo na mkewe hajui, kuna kushauriana tena hapo?

“Lakini mke wa Kafulila ameivua nguo ndoa yao. Mwanamke wa Kiafrika huwezi kujitokeza hadharani na kumsema mumeo kwa maneno hayo, tena mbele ya vyombo vya habari, kwa nini wasizungumzie ndani?


alikuwa Dodoma na Kafulila Dar, wale ni wanandoa wangeweza kuonana kwa namna yoyote na kuzungumza kama ni tofauti zao kuhusu mambo ya vyama, sisi tusingejua tungeamini tu kwamba wameshirikishana, lakini sasa ameanika kila kitu kwamba hakuwa na taarifa, mwanamke hapaswi kuwa hivyo.

“Sasa kazi hiyo hapo, mume ameachana na upinzani na kama atahamia CCM maana yake ni kwamba atakuwa na mapenzi na Magufuli na mkewe aking’ang’ania Chadema maana yake ni kwamba ana mapenzi na Mbowe, hapo hakuna ndoa tena,” alisema mmoja wa wahadhiri wa chuo kikuu kimojawapo cha jijini Dar, baada ya kuulizwa na mwandishi wetu juu ya kauli ya mke wa Kafulila juu ya uamuzi wa mumewe.

SIKIA HII;
Katika kudodosa mambo, mwandishi wetu alizungumza na mmoja wa wabunge wanawake vijana ambaye alisema dalili za Kishoa kupingana na Kafulila zilianza zamani na kwamba hutofautiana mara kwa mara kwa mambo mengi, kisiasa na maisha kwa ujumla.

“Unajua mimi ni rafiki mkubwa sana wa familia yao, wakati mwingine wote wawili hunishirikisha kupishana kwao juu ya mambo mengi na wakati mwingine hutofautiana mbele yangu na mimi kugeuka msuluhishi, Jesca hajaanza leo kupishana na mumewe,” alisema mbunge huyo huku akiomba hifadhi ya jina lake ingawa wahusika wanamjua.

KISHOA ANASEMAJE?
Baada ya kutoa kauli hiyo, mwandishi wetu alimpigia simu mara kwa mara lakini Jesca alikuwa akikata na wakati mwingine kutopokea kabisa.

NINI MSIMAMO WA KAFULILA KUHUSU NDOA?
Hata hivyo, katika kujibu suala hilo, Kafulila alisema kwa kifupi: “Uamuzi wangu hauhusiani na mambo ya ndoa, hayo ni mambo mengine kabisa.”
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. No respect. Kwa wanandoa kutokujali ndoa yao kwa mambo ya kisiasa hapa huwezi tena kumwamini mumeo. Mke wake alimsaidia sana na kusimama naye wakati wa matatizo. Leo anamponda kama mtu asiye na thamani kwa majibu ya aibu kuhusu ndoa yake. Mwanaume kama huyo huwezi kumtegemea ukiwa na shida . Atakubwaga kama aalivyo fanya. Mkewe hakumbwaga alipokuwa anahangaika. Ushauri wangu hapa hakuna ndoa. Mume kisha amua hivyo.. hamthamini mke wake. Angetstua kwanza mambo ya unyumba kabla ya kuhama. Nashangaa mtu wa busara kukurupuka , kuna kitu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad