Nimehama Chadema Lakini Sijahamua Chama cha Kujiunga Nacho- Kafulila

Nimehama Chadema Lakini Sijahamua Chama cha Kujiunga Nacho- Kafulila
ALIYEKUWA mbunge wa Kigoma Kusini tangu 2010-15 na baadaye kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) David Kafulila, amesema kwamba pamoja na kutangaza kukihama chama chake hicho, bado hajaamua chama ambacho atajiunga nacho, lakini akasisitiza kwamba ajenda ya ufisadi aliyokuwa anaipigania upande wa upinzani imetoweka na sasa anatafuta sehemu ya kuiendeleza.

Kafulila aliyasema hayo wakati akihojiwa  jijini Dar es Salaam leo, ikiwa ni siku moja tangu atangaze uamuzi wa kuondoka Chadema.

“Hilo ni jambo la kawaida kwa wanasiasa duniani kuhama wakati wanatetea ajenda zao,” alisema Kafulila ambaye alipata tuzo akiwa mbunge wa kwanza kuendesha harakati  dhidi ya ufisadi  Aprili 29, 2015.

Aliongeza kwamba msimamo wake wa kupiga vita ufisadi tangu utotoni hadi kuingia bungeni uko palepale na atauendeleza akiwa katika chama chochote.

Kuhusu madai  kwamba hana imani na upinzani ambako umeshindwa kupambana na ufisadi, wakati ndipo alipopatumia kujiimarisha katika vita hiyo, mwanasiasa huyo machachari alisisitiza kwamba  ajenda ya kupiga vita ufisadi imekufa katika vyama hivyo na ameona hakuna tena matumaini ya kuifufua ajenda hiyo ambayo awali ilikuwa ndiyo nembo ya upinzani.

Pia Kafulila alikanusha mawazo kwamba ameondoka chama hicho baada ya kukosa maslahi kwa kutopata cheo,  ambapo amesema kama ni vyeo bado nafasi zipo Chadema na watu wanajitokeza kuvigombea, jambo ambalo yeye hakulifanya wakati akiwa huko.  Kwa hiyo, akasisitiza kwamba suala la kutopata cheo katika chama hicho siyo lililomfanya ajivue uanachama.

Hata hivyo, wakati akisubiri chama cha kujiunga nacho, alimsifia  Rais John Magufuli kwamba  amejipambanua katika suala la kuupiga vita ufisadi na anakubalika ndani na nje ya nchi na kwamba watu wengi wanakubaliana na hatua anazozichukua.

Kafulila alikuwa mwanachama wa Chadema baadaye akajiunga na NCCR-Mageuzi, akarejea tena Chadema hadi alipojivua uanachama jana.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. aende tu hakuna namna

    ReplyDelete
  2. Nakuonea huruma dogo. Kati ya watu wengi waliohama nisingetegemea kukuona wewe mmojawapo. Kutokana na uliyoyapitia. Sijui ni safari ulizokwenda nje, lakini kuna kitu nyuma ya pazia juu ya hawa wote wanaohama hasa kutoka chadema. Kuna evil force either kutoka nje au ndani au pande zote kutokana na uwekezaji nchini na mikataba mikuu. Ukiangalia toka dr slaa, kafulila, kiongozi wa bachva unamwona kabisa hana amani. Mpaka itokee kama zimbabwe sasa ndipo watanzania wengi watakuja kuamka na itakuwa too late. Chadema kwa maono yangu ilishachukuadola kwa sasa. Ingawa Lisu ilikuwa afe na ikashindikana sasa wametumia ujanja mwimgine kutaka kukidhoofisha chadema kwa kuwapiga maneno au pesa kwa wale walioonekana majembe.sasa wanaungana na mafisadi ambao hawatatumbuliwa hasa kurudia kulekule kwenye mchezo mchafu. Waumiao ni wananchi hasa vijijini, au mpaka vijana watakapoona hali ngumu zaidi na kushindwa kuvumilia maisha na ikifikia hapo ni hatari kubwa nchini. Huyu aliyesuka mpango mzima si mtanzania peke yake ni nguvu pia za wawekezaji nchini kutaka kuota makucha zaidi kwa kupitia chama tawala na serikali. Na hawa wanaosalimu amri watasaidia kunyima uhuru, kutokuadhibu mafisadi na watapata vyeo shida kwa wale wasio na sauti serikalini, maskini ndo watakuwa maskini zaidi.
    Leo tumeona Migambe ambaye kabiresha elimu kwanza bora kuliko Africa nzima. Lakini wachache na mabepari wameingia ndani ya wazimbabwr kumtoa Mugabe kama mnyama. Shida vijana wamekisa mweleleo. Naamini sana ilikuwa atoke lakini si kwa namna hii. Afrika nzima imeingiliwa tu kwa kuwa watu wetu hawajaona mbali. I had hoped through Chadema lakini aliyewapiga msasa wa uongo kuanzia Slaa, na nyinyi nyote nimekata tamaa ushujaa wa nchi hii hspo. Ni rahisi sana kuingiliwa kisaikologia. Na hii ni hatari sana kwa usalama wa nchi hii. Mafisadi wameshinda na wawekezaji wao. Na watu wamefungwa midomo. Taifa zima linashindwa kuona .

    ReplyDelete
  3. Jamaa sawa na jeshi anaeogopa vita mmjomba kitu kimoja heshima yako imeshuka sio wewe tu wale wote munaotoka upinzani na kurudi milikokua hakuna kilichobadilika ,watu wanapotea hakuna kinachofanyika wakowanaopigwa risasi hukuna kinachotendeka mulikua musimame imara mumelishwa asali mumesahau malengo yenu dah baada ya muda mfupi tz itakua kama Zimbabwe wacha tuone lkn aibu mjomba si bure ipo namna na ukali wote uliokua nao leo imekua hivyo nilikuamini na kukuheshimu lkn umepoteza muelekeo dogo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad