Mshambuliaji wa Manchester United Romelo Lukaku amesema amezaliwa kufunga na anaamini ataendelea kufanya hivyo pamoja na kuvunja rekodi ufungaji bora nchini Ubelgiji kabla ya mwaka huu kuisha.
Lukaku ameyasema hayo baada ya kuifikia rekodi ya Paul Van Himst na Bernard Voorhoof ya mabao 30 katika timu ya taifa ya Ubelgiji, ambapo ameeleza kuwa bado ana nia ya kufunga zaidi.
“Nimezaliwa kwa ajili ya hili na nitaendelea kufanya hivyo", amesema Lukaku ambaye sasa anahitaji bao moja tu kuweza kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wa nchini ya Ubelgiji.
Lukaku alifunga mabao mawili kwenye sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mexico hivyo kufikisha mabao 30 sawa na Paul Van Himst na Bernard Voorhoof ambao wanashikilia rekodi hiyo.
Lukaku anafanya vizuri msimu huu akiwa na Manchester United ambapo tayari amefunga mabao saba kwenye ligi kuu soka nchini England. Lukaku anaweza kuvunja rekodi siku ya jumanne ambapo Ubelgiji itacheza mechi ya kirafiki na Japan.