Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu, Jijini Mwanza katika uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu kwenye kampeni ya kumnadi mgombea udiwani Godfrey Mahame
Godfrey Mahame.
"Nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii ya leo ili nipate fursa ya kupigania mageuzi ya kisiasa na ya kiuchumi Tanzania," amesema Nyalandu baada ya kukabidhiwa kadi.
Amesema ana shauku, furaha na heshima kukaribishwa rasmi kuwa mwanachama wa Chadema. Nyalandu ameongeza kuwa katika majira na nyakati ambazo Taifa linapitia, mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania ni lazima.
"Naungana na chama hiki pendwa ili tutembee pamoja mtaa kwa mtaa kijiji kwa kijiji tuwaambie wananchi wakati wa ukombozi ni sasa," alisema Nyalandu.
"Saa ya mabadiliko imefika kwa mtu yeyote miongoni mwetu, tumepewa utayari wa kubadilisha mwelekeo wa nchi," amesema.
hahahaha! eti nimeisubiri kwa shauku........kwani hicho chama ni kipya?? kwanza hawamkatai mtu alotoma CCM, hasa wale mafisadi, ukihamia kwao utakuwa malaika...tehetehetehe kwa CCM, wezi, mafisadi sasa bhaaassss HAPA-KAZI-TU
ReplyDelete