Nyaya za umeme zenye thamani ya sh. milioni 70.7 zakamatwa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, tarehe 07  Novemba maeneo ya Tegeta IPTL lilifanikiwa kukamata gari lenye namba za usajili T. 897 ARF aina ya Fusso likiwa limebeba nyaya za umeme Roller/Drum 05 zikiwa ndani ya gari hilo zenye thamani ya Tsh Milioni 70.7.

Dereva wa gari hilo aliwaelekeza askari watuhumiwa wenzake na baada ya upekuzi zilikamatwa Roller/drum 02, mashine ya kupaka, rangi na makopo matatu (3)matupu ya rangi yaliyotumika kubadilisha uhalisia wa Roller/drum, zote zilikutwa kwa mtu aitwaye Zawako Kasiba na mke wake, mkazi wa IPTL Tegeta na watuhumiwa wengine wanne.

Aidha watuhumiwa wote wamekamatwa na mawasiliano yalifanyika na Shirika la umeme (TANESCO) na walipofika kuzitambua nyaya hizo na kugundua kuwa ni mali za Shirika ambazo ni DRUM 07 zikiwa na mita 21,000 zenye thamani ya sh. Milioni 70.7

Jumla ya watuhumiwa sita wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo akiwemo mwanamke mmoja. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaotuhumiwa kuhujumu miundo mbinu ya TANESCO.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad