Orodha Nzima ya Makada Mbalimbali Kutoka Vyama vya Upinzani Waliojiunga na CCM Leo


Chama cha Mapinduzi (CCM) leo katika Mkutano wa Kamati Kuu unaofanyikia Ikulu, Jijini Dar es Salaam, kimepokea maombi ya kujiunga na chama hicho kutoka kwa makada mbalimbali wa vyama tofauti vya upinzani.

Pamoja na hayo, pia Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesoma hadharani barua ya maombi ya kurudishwa CCM ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM, Bi Sophia Simba aliyefukuzwa uanachama kwa tuhuma za usaliti.

Makada kutoka vyama mbalimbali vya upinzani walioomba ridhaa ya kujiunga na CCM ni pamoja na Prof. Kitila Mkumbo, aliyekuwa Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo na wakili wa kujitegemea Albert Msando na Lawrence Kego Masha.

Wengine ni aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Patrobas Katambi, aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa ya Chama Cha ACT-Wazalendo Samson Mwigamba pamoja na Katibu wa Kamati ya Programu za Kijamii Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Hlmashauri Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo Edna Sunga.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauto katika mkutano huo, makada hao wameeleza kuwa sababu zilizowapelekea kuvihama vyama vyao na kuomba kujiunga na CCM ni pamoja na kuridhishwa na utendaji kazi wa serikali ya Rais Magufuli, CCM kuirudia misingi iliyowekwa na waasisi, juhudi za kupambana na rushwa na ufisadi, nidhamu na uwajibikaji pamoja na jihudi za kutetea na kupambania maendeleo kwa wanyonge.

Makada hao wameahidi kuonyesha ushirikiano na kukitumikia CCM pamoja na kutoa ushauri katika maeneo mbalimbali ikiwamo kuwashawishi wengine kujiunga na chama hicho pia.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kwa pamoja wameridhia kuwapokea wanachama hao wapya pamoja na kumsamehe Bi Sophia Simba aliyekuwa amefukuzwa uanachama kwa tuhuma za usaliti.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watu kama Masha ingawa wanaakili safi, hawana msimamo wao kamili. Watu kama hawa muwaangalie sana. Wanasema hiki, lakini wanawafuata Wazazi wao na kwa vile ni CCM muda mwingi, na Wanatafuta vyeo tena lazima Warudi tena CCM kwani ndiko wanapeana ajira. Si kwa sababu ya uwezo, bali kutafuta ushindi tu. Si kwa kuwajali Watanzania bali matumbo yao. Ingawa wamesoma nje, na kuwaona watu wa mataifa mengine kuto kuhamahama hawajui What it means to be patriotic. Huwezi kuhamahama ukajiita msomi mwenye msimamo. Unajiingiza huku ukiangalia kilicho mbele yako, kama hakina uhakika unajiuza tena. What a shame. Ni kuhangaika huku na huku. Wengi wamemuona Mbowe mgonjwa hawajui nguvu za Mbowe na Mungu. Watakuja kujiaibisha. Ni ndumila kuwili watafutao cha haraka bila investment yeyote.
    Hamna kipya. Vijana Waogopeni sana hawa watu, wameshapewa madaraka na wameshiba.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad