Papa Francis Apiga Marufuku Uuzaji wa Sigara Vatican

Papa Francis Apiga Marufuku Uuzaji wa Sigara Vatican
Papa Francis ameagiza marufuku ya uuzaji wa sigara ndani ya Vatican , kuanzia mwaka ujao.
Msemaji wa Vatican Greg Burke alisema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubali na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu.
Takriban wafanyikazi 5000 wa Vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua sigara zilizopunguzwa bei .
Papa Francis asogeza mbele kusamehewa kwa wanaotoa mimba
Papa Francis awataka makasisi Nigeria wamtii
Papa Francis aomba msamaha kwa mauaji Rwanda
Mauzo hayo yanakadiriwa kuiletea Vatican mamilioni ya yuro kila mwaka.
Lakini bwana Burke amesema kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu.
Alinukuu takwimu za shirika la afya duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka.
''Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa sababu ya ufadhili wanaopata'' ,alisema.
''Ni kitu ambacho ni lazima kufutilia mbali licha ya kuleta mapato Vatican, muhimu ni kufanya kile kilicho sawa''.
Papa Francis ambaye pafu lake moja liliondolewa wakati alipokuwa kijana havuti sigara.
Wafanyikazi wa vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua pakiti tano za sigara kila mwezi kutoka kwa duka lisilotozwa ushuru.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad