Papa Francis amewasili nchini Myanmar kwa ziara ya wiki nchini humo na Bangladesh, wakati wasiwasi unaendelea wa kimataifa kuhusu usalama na ulinzi kwa wasilamu wa Rohingya.
Lengo ni kuona iwapo atatumia neno "Rohingya" kuwaita kundi la watu wanaosema wamenyanyaswa.
Maafisa nchini Myanmar wanakataa kulitumia jina hilo, jambo ambalo linaongeza wasiwasi kwamba huenda kukazuka ghasia za Mabudda walio wengi nchini humo iwapo Papa atalitumia jina hilo.
Hata kabla ya kuondoka Roma, Papa Francis alikuwa anakabailiwana kitendawili cha kidiplomasia: iwapo kuliita kundi dogo la waislamu Myanmar - Rohingya.
Ni jina lisilo tumika na serikali ya kiraia na jeshi - wakieleza kuwa ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh na kwahivyo hawapaswi kuorodheshwa kama mojawapo ya makabila nchini humo.
Lakini mashirika ya kutetea haki za binaadamu wanamuomba awaite hivyo, yakieleza kuwa nilazima Papa Francis aoneshe huruma kwa watu walionyimwa uraia na tangu Agosti wamekabiliwa na kile kamishna wa haki za binaadamu katika Umoja wa mataifa amekitaja kuwa 'kinachoonekana kuwa mauaji ya kikabila'.
Zaidi ya WaRohingya 600,000 wamekimbilia mpakani - na wakimbizi wakielezea kukabiliwa na mauaji, ubakaji na kuteketezwa moto kwa vijiji - jeshi imekana tuhuma zote.
Papa atakutana na kiongozi wa Myanmarr - Aung Sun Suu Kyi - Jumanne - huenda ni jukumu zito kidiplomasia katika miaka yake minne kama kiongozi wa kanisa katoliki.
Papa Yuko Myanmar Inayotuhumiwa kwa Mauaji ya Waislamu wa Rohingya
0
November 27, 2017
Tags