Polisi Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi

Polisi Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamtuhumu Dk. Louis Shika, kutumiwa na mfanyabiashara Said Lugumi, ili kukwamisha uuzwaji wa nyumba zake zinazoshikiliwa na serikali.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ameeleza wanatilia shaka kuwa mtuhumiwa alitumwa na Lugumi kukwamisha mchakato wa mnada, kwani mazingira ya mnada, na namna mtuhumiwa aliyokuwa anataja bei yanawafanya kuamini kuwa aliwekwa ili wanunuzi wengine wasiweze kununua nyumba hizo.

“Aliwekwa na Lugumi mwenyewe ili mnada usifanyike ingawa sina fact za kudhibitisha hilo, ila alichokuwa anakifanya kinatufanya tuamini hivyo. Alikuwa ana-top bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,” amesema Mambosasa.

“Ila jinsi alivyo, kwa maana ya uvaaji na kuongea kwake watu walitia mashaka kama ataweza kununua ndipo akatakiwa kutoa asilimia 25 na kushindwa kulipa. Tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano,” aliongeza na kusema jeshi hilo linaendelea kumshikilia Louis kwa mahojiano zaidi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad