MWANAZUONI maarufu barani Afrika, Profesa Patrick Lumumba, amesema Rais Dk. John Magufuli na Rais wa Rwanda, Paul Kagame si madikteta bali wanachokifanya ni kuhakikisha kunakuwa na siasa za miiko na maadili.
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana katika Mkutano wa Pan African Humanitarian wa mwaka huu ulioandaliwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (Yuna) uliokuwa na kaulimbiu ya “amani inawezekana jana, sasa na kesho” na kuwakutanisha vijana kujadili nafasi zao katika kuleta amani barani Afrika.
Profesa Lumumba ambaye ni raia wa Kenya, alisema katika miaka ya hivi karibuni, wamekuja viongozi wenye mwelekeo na uchungu wa kuhakikisha mataifa yao yanaendelea, lakini baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwaita madikteta.
“Tunapaswa kujua hawa watu tunaowaita madikteta ni akina nani, kwa sababu kuna viongozi wameibuka katika miaka mitatu hadi 20 iliyopita, wakiwa na mwelekeo na kuona uchungu wa kuhakikisha mataifa yao yanaendelea, lakini baadhi ya watu wengine wanawaita eti ni madikteta,” alisema na kuongeza:
“Lakini viongozi hao ni watu wazalendo na wakereketwa wa maendeleo endelevu, hivyo watu kama hawa lazima tujiulize mienendo yao ni ya kidikteta? Au ni ya kuhakikisha mataifa yao yanapiga hatua za haja na hoja. Mfano wengine wanasema Kagame, Dk. Magufuli ni dikteta, sikubaliani nao kwa sababu kile ambacho wanakifanya, wanajaribu kusema kwamba lazima kuwe na siasa za miiko na maadili.
“Nakubali kwamba udikteta ni jambo ambalo halistahili, lakini ni muhimu kuhoji kwamba uhuni ndiyo demokrasia? Kwa sababu kumeibuka wimbi la watu ambao ni wababaishaji hata sio wapinzani, kila kitu anachokifanya (rais) wao kazi yao ni kupinga.”
Akizungumzia suala la amani, hasa katika vipindi vya uchaguzi, alisema ni wakati wa kujiuliza ni aina gani ya uongozi inahitajika barani Afrika ili kuwe na njia ya kubadilisha uongozi isiyoleta vurugu tofauti na ilivyo sasa.
“Pia tunapaswa kuangalia hivi vitu tunavyoviita vyama, ni vyama kweli au ni vikundi tu, genge tu la vibarua waliokuja kujitafutia nyadhifa ili kupora mali za Waafrika. Vijana ndio wataibua hoja hii na kutathimini kuwa mataifa yetu tunayaandaa kwa minajili ya kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo,” alisema.
Pia alisema anaamini Afrika itakuja kuwa na amani na utulivu kwa sababu jitihada mahsusi zimeshaanza kufanywa na viongozi wake na tayari wamekwisha kutoa tamko kwamba kufikia mwaka 2020, lazima vitu vinavyoleta migogoro vitolewe na kila mtu anatakiwa kushiriki kwa nafasi yake.
Mtanzania
Lumumba aache kuingilia mambo ya ndani na kuwa mchochezi kwa manufaa binafsi.Ulishindwa Kenya sasa unaingilia mambo yasiyokuhusu.Waache vijana wawe huru na si kuwavuruga kiakili. You are more British than British themselves. Ukasumba na usiasa badala ya uzalendo.aceni kuiga ya wenzenu mjisikie huru na majivuno kama waafrika wazalendo kwa misingi ya africa.Madictata wanavunja maadili na huyu Mtanzania amevunja maadili.kutumia nguvu kuna madhara yake. Kutoa uhuru, kukubali ushauri no mbinu ambazo sisi waafrika tujifunze ili kuudumisha uhuru.woga, kutokujiamini kwa viongozi ndiko kunawafanya kutumia ubabe. Fikra binafsi za kujifikiri kwa kuwa upo raisi mawazo yako ni sahihi kupita watanzania wote, huu ni udictata. Na dictata mara nyingi anafikiri yeye tu ndo mkombozi. Kiongozi bora ni yule anayechukua mawazo na ushauri wa wengi. Ni wachache sana wenye uwezo binafsi kuwa sahihi kiuongozi. Na viongozi wote wanaofanikiwa duniani ni wale wasikivu, humble na si wanaojitwalia nguvu mkononi. Nakushangaa mwanasheria kama wewe kutwist mambo.Na haya yanamadhara sana duniani. Ndo maana ulishindwa kenya, ilikuwa densi ya kiingereza kubwa badala ya kutumia hekima .it was a big dance of proper english versus facts.na unarufia tena. Ni kujitafutia sifa na unora lakini ni upotoshaji wa sheria.
ReplyDeletehiyo hotuba umemwandikia nani kama siyo uzwazwa??? kaa pembemi na jifunze kuandika, unaonekana ni mchovu wa akili
DeleteSwadakta ProffeSa Lumumba...unayosema Ni kweli kwa mmenue Akili na muelewa.
ReplyDeleteWapuuI na wente magenge watakupinga na kujifanya hawaluelewi.
Hai ndio zao.
Hongera kwa mtazamo Wako WA ukweli.
Mungu Baba akubariji kwa uchambuzi huu na kutuamshia vijana toka njia ya upotoshwaji.
LONG LIVE AFRIKA.
Non sense. Kuna mawakili wengi Afrika walioelimika UK na mfumo wa huko. They need to examine themselves and help Africa end this kind of dictatorship. One person mind set for all.powers which has no place in this century. You cant declare saviour with one monopoly mindset for millions without the ability.accept criticism and challenges from others believing you know all. Truth must be sad to prevent more disasters instead of sugar coating the person. Be truthful instead.
ReplyDelete